Jumapili, 26 Julai 2015

JASHO LA MTU HALILIWI, CHEZEA NDNDO WE????????

Kikosi cha Makarwe Fc  kikiongozwa na captain Charles watatu (kushoto) kabla ya kukwaanana Muleba stendi fc hapo jana katika kiwanja cha vijana wilayani Muleba.

Kikosi cha Muleba stend  fc kiongozwa na captain Matov John wa pili kutoka kulia ( waliosimama) kabla ya kuumana na Makarwe fc hapoa jana katika nyasi za Uwanja wa Vijana wilayani Muleba.

Baadhi ya vijana chipukizi katika medani ya soka kuanzia kushoto Mukusin ,Afidhu(katikati) na mwisho kulia Kpilima, waki wakilisha timu yao ya Muleba stendi dhidi ya Makarwe hapo jana.

Mmoja wa waendeshaji wa blog hii Majid Y. Abdulkarim akipata picha na baadhi ya wachezaji wa Muleba stendi kabla ya kukiputa na Makarwe fc kwenye mchezo wa jana Muleba stendi ilipata ushindi wa bao tano kwa bila.

Kipaji cha mtu ni ajira yake tosha!!







Waamuzi wa mchezo wa Makarwe fc dhidi ya Muleba stendi baada ya kukagua timu wakijipanga kuliwasha kwa dakika 90 hapo jana.



Unaposema beki hana sifa basi kijana huyu ndo kazi yake mwanzo mwisho dakika 90 ndo pumzi yake.

BENCHI LA UFUNDI LA MULEBA STENDI FC

Midfielder wa Muleba Stendi fc Maurid( Midfielder kisheti Maula) akipoza koo.



Striker Nikison (watatu kutoka kushoto) anayetambua wajibu awapoa dimbani wake mechi 4 na mabao 4.









LEO TENA!!!!!!!!!!!!!!!



Na Saleh Ally
Robo fainali ya Kombe la Kagame itakayopigwa Jumatano ndiyo itakuwa tamu kuliko zote msimu huu.


Inazikutanisha timu mbili za Tanzania, Yanga dhidi ya Azam FC.

Mechi hiyo, hata kabla haijachezwa, tayari imezaa lundo la burudani ambazo zina maswali mengi.

Kwanza kabisa ni Tanzania kuwa na uhakika wa timu itakayotinga nusu fainali, yaani timu nne za mwisho.

Ikiwa Azam au Yanga, moja wapo itakuwa na kazi ya kucheza mechi moja zaidi ili itinge fainali na baada ya hapo ni ‘mipango’ ya ubingwa.


Kinachovutia zaidi ni suala la mashabiki wengi wa Simba ambao wamekuwa wakizishangilia kila timu zinazokutana na Yanga hasa katika michuano ya Kagame.

Mashabiki wengi wa Simba hujitokeza kwa wingi kuizomea Yanga na kumshangilia mpinzani wake.

Lakini safari hii, Yanga inakutana na Azam FC. Si kwamba ni timu ya Tanzania ndiyo maana Simba wataishangilia au watahofia kuizomea, lakini hata Azam FC nao wanaonekana kuwa ‘wasaliti’ kwa Simba.

Hali hiyo inatokana na ule uamuzi wa mechi ya mwisho ya msimu, wakati Yanga tayari ni mabingwa na Simba na Azam FC wakiwania nafasi ya pili.

Azam FC alikuwa na asilimia 75 ya kupata nafasi hiyo huku Simba wakibaki na 25 lakini hawakukata tamaa.
Mechi iliyokuwa inatakiwa kuamua ni kati ya Yanga dhidi ya Azam FC. Kama Azam ingefungwa na Yanga, basi ingeibua matumaini ya Simba na ile asilimia 25 ingepanda.
Lakini Yanga ikalala, Simba wakaona kuwa kulikuwa na ‘mipangp’. Tena wakaalani kulikuwa na mvua kubwa lakini bado mechi iliendelea kuchezwa kwa kuwa Azam FC walikuwa wanaongoza na mwisho walishinda.

Kilichowaudhi zaidi, Simba ambao angalau walionekana na ‘undugu’ na Azam FC kuliko Yanga, ni kuona Yanga na Azam kwa pamoja wakiwa wameungana na kushangilia mara tu baada ya mechi.

Mashabiki wenye njano na kijani, waliunga na wenye nyeupe na bluu na kuangusha bonge la ‘sherehe’ pale Taifa tena bila ya kujali mvua.

Sasa Simba wataishangilia Azam FC iiue Simba, au kwa mara ya kwanza wataweka rekodi kuizomea Yanga pamoja na timu wanayocheza nayo.

Je, ule urafiki wa Yanga na Azam utakuwepo tena Jumatano? Watashangilia pamoja tena au sana nao ni ‘maadui’?


Hii ni sehemu ya kuonyesha soka lilivyo na burudani na huenda, Jumatano kutakuwa na burudani ya kutosha ndani na jukwaani kwenye Uwanja wa Taifa.

Barcelona wachabangwa 3 na Manchester united




 
Wayne Rooney, Jesse Lingard na Adnan Januzaj ndio waliotikisa  nyavu  katika ushindi dhidi ya mabingwa wa Ulaya Barcelona.
Wayne Rooney alifunga bao kwa Manchester United dhidi ya Barcelona baada ya dakika tu 8 kwenye Uwanja Lawi
Rafinha alifunga la kufutia machozi marehemu kwa ajili ya Barcelona kabla Adnan Januzaj alifunga kwaUnited katika dakika za majeruhi 

(chanzo dailymaily.co.uk)  Red Devils playmaker Juan Mata plays a forward ball during United's International Champions Cup clash against the Spanish giants
Barcelona forward Luis Suarez attempts to bend the ball around the Manchester United wall during Saturday's friendly at Levi's Stadium

Jumamosi, 25 Julai 2015

HICHI NDICHO ALICHO KISEMA KANAVARO KUHUSIANA NA SIMBA KUMSAJILI OLUNGA

Simba inapambana muda wote kuhakikisha inamsajili straika Michael Olunga wa Gor Mahia, lakini nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ni kama anataka kutibua dili hilo aliposema; “Huyo Olunga hana lolote, isipokuwa ana bahati tu.”


Cannavaro alienda mbali kwa kusema, siku Yanga ilipocheza na Gor Mahia ni kweli Olunga aliwasumbua na kufanikiwa kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-1 walioupata, lakini hana uwezo wa kusumbua katika ligi.
CANNAVARO
Cannavaro amesema: “Ujue siku ile tulipocheza na Gor Mahia, Olunga alikuwa na bahati na kweli alitusumbua lakini sidhani kama ana uwezo mkubwa kiasi cha kututisha.”

“Kwa kweli alibahatisha tu, nasikia Simba wanataka kumsajili. Waache wamsajili halafu tukutane naye katika ligi (Ligi Kuu Bara) ndipo watakapoona kama wanamsajili mchezaji wa kawaida tu.”


Cannavaro alisema anatamani wakutane tena na Gor Mahia katika mechi zijazo za Kombe la Kagame ili kuthibitisha kauli yake na kuwahakikishia Simba kwamba wanataka kusajili mchezaji wa kawaida.

Jumatatu, 20 Julai 2015

Blatter atupiwa pesa Zurich

Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter ametupiwa pesa na mtu aliyevamia mkutano wake na wanahabari.
Mvamizi huyo aliyetambuliwa kama Lee Nelson raia wa Uingereza aliondolewa ukumbini humo mara moja na maafisa wa usalama wa FIFA.
Blatter aliyekuwa ameudhika sana na tukio hilo alisema 'halikuhusiana kwa njia yeyote na kandanda' kabla yake kuondoka ukumbini.
Blatter alitangaza mabadiliko kadha ikianza na tarehe ya uchaguzi ambayo itakuwa mwezi Februari mwakani.
nullMvamizi huyo aliyetambuliwa kama Lee Nelson ni raia wa Uingereza
Aidha Viongozi watakaokuwa na ari ya kurithi kiti hicho cha rais wa FIFA,sharti wawasilishe rasmi maombi yao kabla ya tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu.
Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya (Uefa) Michel Platini, anadaiwa kupata shinikizo kutoka kwa viongozi wengi wa bara hilo kuwasilisha ombi lake la kuwa rais wa FIFA.
Mkutano huo wa leo pia ulitaja baadhi ya mambo yatakayorekebishwa ikiwa ni pamoja na kuweka kikomo cha muhula cha urais na viongozi wengine wa ngazi ya juu wa shirikisho hilo.
nullAidha FIFA itateua jopo la watu 11 watakaoanza uchunguzi
Hatua ya kuchapisha mishahara na marupurupu ya viongozi wa ngazi ya juu wa shirikisho hilo pia ilijadiliwa.
Aidha FIFA itateua jopo la watu 11 watakaoanza uchunguzi wa kina kubaini njia za kukabiliana na rushwa na ubadhirifu.
Jopo hilo maalum ndilo litakaloendesha mabadiliko katika Fifa.

(chanzo bbcswahili.com)

HUU NDIO UZI MPYA WA CHELZEA


Chelsea have released their new away kit for the 2015-16 Barclays Premier League seasonChelsea imetambulisha jezi mpya ambazo watazitumia katika msimu mpya wa 2015-16 katika Ligi Kuu ya England ambayo imedhaminiwa na Yokohama Tyres.Chelsea kwa sasa iko katika  ziara nchini Marekani,na  mabingwa hao wa Uingereza wanakabiliwa na kibarua kizito kutoka katika klabu ya uhispania Fc Bacelona  Julai 28, huko Washington marekani.Premier League champions Chelsea will debut the kit during their pre-season tie with Barcelona next weekThe English champions wore white during their Champions League-winning season in 2012http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3167941/Chelsea-release-new-away-kit-champions-prepare-Premier-League-title-defence-debut-white-strip-against-Barcelona.html

Jumapili, 19 Julai 2015

CECAFA:Gor Mahia yainyamazisha Yanga

Mabingwa wa ligi ya soka nchini Kenya Gor Mahia walitoka nyuma na kuinyamazisha timu ya yanga kutoka Tanzania 2-1 katika mechi yao ya ufunguzi wa kombe la CECAFA katika uwanja wa kitaifa wa Dar es Salaam.
K'Ogalo kama wanavyojulikana walikabili tishio la Yanga baada ya beki Dirkir Clay kujifunga mwenyewe na kuweza kufunga mabao mawili kupitia Harun Shakava na mshambuliaji Michael Olunga katika mechi ya kusisimua ambapo Yanga ilimaliza ikiwa na wachezaji 10 uwanjani.
Shakava alifunga bao la kusawazisha baada ya kufunga kichwa kizuri kutoka kwa mkwaju wa adhabu uliopigwa na Karim Nizigiyimana baada ya Godfrey Walusimbi kuangushwa upande wa kushoto kunako dakika ya 18 kabla ya Olunga kuimarisha mambo na kuiweka Gor kifua mbele dakika moja baada ya kipindi cha mapumziko.
Nahodha wa timu ya Yanga Nadur alikosa penalti katika kipindi cha pili baada ya Shakava wa Gor Mahia kuunawa mpira katika eneo la hatari huku kipa wa Gor Mahia akiudaka mkwaju wake kwa urahisi.
Katika mechi nyingine ya ufunguzi, KMKM ya Zanzibar waliwafunga Telecom ya Djibouti 1-0 katika uwanja wa kumbukumbu ya Karume.
APR ya Rwanda pia iliwafunga Al-Shandy ya Sudan 1-0 katika mechi iliyoanza kabla ya ile ya Yanga vs Gor Mahia katika uwanja wa Taifa.
Sehemu ya ratiba ya michuano hiyo inayodhaminiwa na Raisi wa Rwanda, Paul Kagame ni kama ifuatavyo:

chanzo bbcswahili.com

Jumamosi, 18 Julai 2015

BINGWA BALA ALAMBA 2 -1

MUUAJI WA YANGA: OLUNGA, NI HATARI...
Yanga imepoteza kwa bao 2-1 katika mechi ya ufunguzi ya Kombe la Kagame.
Gor Mahia, mabingwa wa Kenya ndiyo walioibuka na ushindi katika mchezo huo mtamu uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 katika kipindi cha kwanza.

Lakini Gor Mahia wakazidi kutamba katika kipindi cha pili kwa kupata bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Michael Olunga.

Olunga aliyekuwa akiisumbua ngome ya Yanga tokea kipindi cha kwanza alifunga bao hilo baada ya kuwatoka Kelvin Yondani na Mbuyu Twite.

Yanga walitangulia kupata bao katika kipindi cha kwanza baada ya Gor Mahia kujifunga baada ya krosi ya Donald Ngoma, hiyo ilikuwa dakika ya 5.

Dakika ya 16, Shakava akasawazisha kwa kichwa baada ya Juma Abdul kumuangudha Walusimbi.
Dakika ya 24, Ngoma akalambwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje.

Nahodha Nadir Haroub Cannavaro alikuwa na nafasi ya kusawazisha kwa Yanga baada ya kupiga mkwaju wa penalty, kipa akaudaka.


Mwishoni mwa kipindi cha pili Yanga walicharuka na kushambulia mfululizo lakini haikuwazuia Gor kukomaa na kubakiza ushindi wao wa kwanza dhidi ya Yanga.




Mshambuliaji mwenye minguvu wa Simba, Elius Maguli, ameonekana kujiamini kupitiliza baada ya kutamka kuwa atafanya kazi yake kwa ufasaha na kuwazidi ujanja Laudit Mavugo na Khamis Kiiza ili yeye awe bora zaidi yao.

Maguli ameenda mbali zaidi kwa kusema, yeye ndiye mbadala wa straika Emmanuel Okwi aliyejiunga na Klabu ya Sonderjyske ya Denmark na siyo mchezaji mwingine yeyote.

Tayari Kiiza ameshajiunga na Simba lakini Mavugo bado yupo kwao akimalizia mechi za timu yake ya Vital’O ndipo aje nchini kujiunga na Wekundu wa Msimbazi.

Maguli alisema haangalii rekodi bali anasubiri kuona uwezo utakaoonyeshwa na wachezaji hao na atapambana nao kwa kufanya mazoezi ya nguvu kuwapiku.

“Unadhani nitaangalia eti nani kafanya nini? Siogopi lolote kwa hao jamaa ninaogombea nao namba, mimi nitapambana kwa mazoezi binafsi na tukikutana kwenye mazoezi ya wote watauona moto wangu,” alisema Maguli.

Hadi sasa Mavugo anaelezwa kufunga mabao 34 katika msimu unaomalizika huko Burundi katika michuano yote na uwezo wa kufunga wa Kiiza unafahamika tangu alipokuwa Yanga msimu uliopita.



Mwanasiasa maarufu wa Kenya, Raila Odinga leo anatarajiwa kushuhudia mechi ya ufunguzi ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame itakayozikutanisha Yanga na Gor Mahia ya Kenya kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Odinga ambaye ni kiongozi wa Chama cha Orange Democratic Movement (ODM)’ ni shabiki mkubwa wa Gor Mahia atakuwa sambamba na baadhi ya mashabiki wa timu hiyo waliosafiri kutoka Kenya kuja kuishangilia.
ODINGA...

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, Odinga ambaye anayedaiwa kuwa na urafiki na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, atatazama mechi hiyo kisha atakutana na baadhi ya wanasiasa na wafanyabiashara wa Tanzania.

Urafiki wa Magufuli na Odinga umethibitishwa zaidi hivi karibuni ambapo waziri huyo aliyechaguliwa kuwania urasi wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kwenda Kenya katika mazishi ya mtoto wa Odinga pia aliwahi kumuunga mkono katika kampeni za urais.

Pamoja na urafiki wake na Magufuli, Odinga ni rafiki wa karibu wa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ambaye imeelezwa huenda akaungana nao uwanjani katika mechi hiyo.

Manji aliwahi kumualika Odinga wakati wa ufunguzi wa maduka yake makubwa ya kibishara ya Quality Centre jijini Dar es Salaam.


Mambo yameshaharibika kwani lile dili la kiungo Ryan Burge kutaka kuwek a rekodi ya kuwa Muingereza wa pili kucheza Ligi Kuu Bara limeshindikana na muda wowote ataondoka nchini kurudi kwao.

Kally Ongala, ndiye raia wa kwanza wa Uingereza, kucheza Ligi Kuu Bara alipozichezea Yanga na Azam, kabla ya kuachana na soka na sasa ni kocha.

Burge alisema: “Mambo yameshindikana na nitarejea nyumbani ambako nimepata timu ya kuchezea, sijajua ni kitu gani kilichokwamisha usajili wangu.”
WANGA (MBELE) WAKATI AKIWA EL MERREIKH AKIPAMBANA NA MIGI WAKATI AKIICHEZEA APR.
Taarifa zinaeleza baada ya ujio wa Allan Wanga, Azam FC imeona ni vizuri kumchukua Mkenya huyo na kuachana na Mwingereza huyo.


Burge alisema: “Muda wowote nitaondoka kurejea nyumbani kwa sababu kuna timu imetokea kunihitaji, siwezi kukutajia ni timu gani mpaka nitakapofika huko na kufanya nao mazungumzo.”

Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo huo bila shaka ataiunga mkono Yanga ambayo ni Tanzania.





Alhamisi, 9 Julai 2015

Manchester United bado wanaendeleza sagura sagura ya usajili na sasa wanataka saini ya mchezaji wa Southampton Morgan Schneiderlin.

 

Manchester United are heading back to Southampton to thrash out a deal for Morgan Schneiderlin (left)Manchester United wataiingia katika mazungumzo na Southampton juu kumnasa Morgan Schneiderlin. Sportsmail wanaeleza kuwa   mwakilishi wa klabu Old Trafford alisafiri hadi pwani ya kusini katika siku ya  Jumatano katika jitihada za kukamilisha mikataba wa mchezaji huyo wa timu ya taifa ya ufaransa.
United wanadhaniwa kuwa kuwasilisha kitita cha  £ 20million kwa ajili ya Schneiderlin
Bosi wa mashetani wekundu  Louis van Gaal anataka kumchukua Schneiderlin kutua  United kabla ya msimu wa  ziara ya Marekani.
chanzo (dailymail.co.uk)http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3154042/Manchester-United-head-Southampton-Morgan-Schneiderlin-deal-pre-season-tour.html

Jumatatu, 6 Julai 2015

Cristiano Ronaldo amegoma kuongea juu uhamisho wa Sergio Ramos kwenda manstester united

Sergio Ramos of Real Madrid celebrates scoring their first goal in stoppage time during the UEFA Champions League Final between Real Madrid and Atletico MadridCristiano Ronaldo amegoma kuongelea juu ya suala la nyota mwenzie Sergio Ramos kutaka kuhama na kuelekea katika klabu aliyo hama ya Manchester united.
Ramos amefikia karibu kuhama katika klabu yake ya real madrid na kulekea
Old Trafford baada ya kutokuelewana na baadhi ya viongozi wa  Bernabeu.
Ronaldo alionekana mwenye hasira alipoulizwa kuhusu Ramos, akisema: "Sijui, mimi sijui"
Wakati nyota wa Ureno alionekana kuchanganyikiwa baada ya waandishi wa habari kumtaka ate maoni yake juu ya uhamisho wa
Sergio Ramos ambao unaonekana kuelekea kufanikiwa. (chanzo mirror.co.uk ).http://matatachede.blogspot.com/2015/07/cristiano-ronaldo-amegoma-kuongea-juu.html