Jumatano, 25 Machi 2015

leo tena



                     Tambwe siri ya mabao



Tambwe alisema kasi waliyonayo sasa imechangiwa kwa kiasi kikubwa na hali ya utulivu iliyopo kwa timu hivi sasa jambo linalowafanya wacheze bila presha na umakini mkubwa.

Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe ametoa siri ya safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kufanya vyema kwenye mechi mbalimbali za hivi karibuni.


Tambwe alisema kasi waliyonayo sasa imechangiwa kwa kiasi kikubwa na hali ya utulivu iliyopo kwa timu hivi sasa jambo linalowafanya wacheze bila presha na umakini mkubwa.

Alisema mchezaji anapokuwa na mambo yanayomvuruga nje au hata ndani ya uwanja, anaondoka mchezoni na kama mshambuliaji ndiyo hujikuta wanakosa mabao mengi ya wazi kutokana na kutokuwa sawa kisaikolojia.


Tambwe aliongeza kuwa jambo lingine linalowafanya wacheze vizuri kwa sasa ni umoja na ushirikiano uliopo baina ya wachezaji wa timu hiyo pamoja na kila mtu kutekeleze majukumu yake ndani na nje ya uwanja.


“Viungo na mabeki wanafanya kazi nzuri kuhakikisha tunafunga mabao. Hili ni jambo ambalo linatuhamasisha washambuliaji tupambane ili ufunga mabao mengi tusiwachoshe wenzetu ambao wanafanya kazi kubwa kuzuia tusifungwe na kutuchezesha,” alisema Tambwe.


Tambwe alimsifu Kocha wa Yanga, Hans Pluijm kwa jinsi alivyoweza kubadilisha kiwango cha wachezaji wa timu hiyo ndani ya kipindi kifupi na amekuwa akiwalea kama watoto wake jambo linalofanya wazidi kuwa na kiu ya kufanya vizuri. Katika hatua nyingine Tambwe alisema Simba itamlipa fedha zake wakati wowote kutoka sasa.


“Viongozi wa Simba wamewasiliana na mimi ili waanze mchakato wa kunilipa, ni jambo la kushukuru kwa kuwa waungwana kwenye suala hili,” alisema Tambwe






                   Mbeya City kucheza na vigogo

 

Mbeya City iliyopoteza makali yake ya msimu uliopita kwa sasa ipo katika nafasi ya tisa ikiwa na pointi 23, imebakiwa na michezo saba kati ya hiyo italazimika kupata matokeo mazuri dhidi ya Azam, Yanga na Simba ndani ya siku 11.


Mbeya City itabidi ifanye kazi ya ziada kuhakikisha inabaki kwenye Ligi Kuu Bara kwani inakutana na mechi tatu ngumu ndani ya siku 11.


Mbeya City iliyopoteza makali yake ya msimu uliopita kwa sasa ipo katika nafasi ya tisa ikiwa na pointi 23, imebakiwa na michezo saba kati ya hiyo italazimika kupata matokeo mazuri dhidi ya Azam, Yanga na Simba ndani ya siku 11.


Mbeya City itacheza na Azam Aprili 8 kisha itaikabili Yanga Aprili 11 mechi zote zitachezwa jijini Dar es Salaam itamaliza na Simba Aprili 18 kwenye Uwanja wa Sokoine. Baada ya kumaliza mechi hizo Mbeya City itaikabili Kagera Sugar, Prisons na Polisi Morogoro mechi hizo zote zitachezwa kwenye Uwanja wake wa nyumbani wa Sokoine Mbeya.


Kocha wa timu hiyo Juma Mwambusi alikiri kuwa anakabilriwa na hali ngumu kwa kuzikabili timu hizo tatu kubwa kwenye Ligi Kuu Bara, lakini wamejiandaa kwa lolote.

“Kweli si mchezo kukutana na timu tatu kubwa kwa muda mfupi na ukiangalia wao wanapambana juu kutwaa ubingwa wakati sisi huku tunatafuta nafasi ya kubaki kwenye ligi, tumejiandaa na tunaendelea


kujiandaa kwa ajili ya mechi zote zilizo mbele yetu na hatuna hofu, tutapambana na tutajua mwisho itakuaje,” alisema Mwambusi








Hakuna maoni: