Taifa Stars kukipiga na Swaziland:COCAFA
Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeendelea na mazoezi katika uwanja
wa Olympia Park kujiandaa na mchezo wa fungua dimba dhidi Swaziland
katika michuano ya COSAFA
Kocha mkuu wa timu ya Taifa Stars Mart Nooij amesema vijana wake wanaendelea vizuri na mazoezi, ikiwa leo ni siku ya pili.
kocha
Nooij amesema hali ya uwanja ni nzuri, uwanja una nyasi nzuri hali
inayopelekea kikosi chake kufanya mazoezi katika mazingira mazuri.
Akiongelea
mchezo wake wa kwanza wa ufunguzi dhidi ya timu ya Taifa ya Swaziland
utakaochezwa siku ya jumatatu, amesema anawajua Swaziland ni timu nzuri,
mara ya mwisho katika mchezo wa kirafiki walitoka nao sare, hivyo
anawaandaa vijana wake kupata ushindi katika mchezo huo.
Kikosi
cha Swaziland kina wachezaji mchanganyiko wakiwemo wanaocheza ligi ya
nyumbani na baadhi wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini.
Taifa Stars itacheza mchezo wa kwanza dhidi ya Swaziland katika Uwanja wa Olympia Park siku ya jumatatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni