Ijumaa, 14 Agosti 2015

KAMPUNI ya Azam Media leo imezindua rasmi chaneli yake mpya yenye ubora wa juu kabisa, iitwayo “Azam Sports HD”.Tangu kuanza kwa huduma za AzamTV, wateja wamekuwa wakijiuliza hasa ni kipi wanachopata kutokana na alama ya HD iliyo mbele ya kisimbuzi – kuanzia sasa watabaini. 
Baada ya miezi 18 ya mipango na uwekezaji, leo umeshuhudiwa uzinduzi wa chanel ya kwanza itakayowezesha wateja kufaidi picha na sauti zaubora wa juu kabisa “HD” kutokana na teknolojia ya kiwango cha juu. 
Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam TV, Tido Mhando akizungumza katika hafla hiyo


Mtendaji Mkuu wa Azam TV, Rhys Torrington akizungumza katika hafla hiyo

Waalikwa mbalimbali wakifuatilia zoezi hilo
Wateja wa kifurushi chenye chaneli mpya ya “Azam Sports” wataweza kuona timu zao wazipendazo katika VPL katika picha ang’avu zaidi ambazo hazijawahi kuonekana. 
Zaidi, kampuni pia imetangaza rasmi ujio wa Ligi Kuu ya Hispania maarufu La Liga ambayo wateja wataipata katika ubora wa HD kupitia Chanel mpya. Mchezo wa kwanza kuoneshwa katika msimu mpya wa La Liga 2015/16, ni Malaga dhidi ya  Seville wa Ijumaa Agosti 21, 2015 na timu zote vigogo zitakuwa zikicheza na kuoneshwa Live mwisho wa juma lijalo, na kila mzunguko wa msimu mzima katika ubora wa HD. 
Mkuu wa Idara ya Masoko ya Azam Media, Mgope Kiwanga akizungumza wakati wa hafla hiyo


Waalikwa mbalimbali wakati wa zoezi hilo leo

Maofisa wa Azam TV wakijadiliana mambo wakati wa shughuli hiyo

Kifurushi kinachojumuisha chaneli ya Azam Sports HD kitaonekana kwa watazamaji wa AzamTV wa Tanzania pekee ambao wanalipia kifurushi chochote kati ya vitatu vya sasa; Pure, Plus au Play – na nyongeza ya ya SH15,000 kwa mwezi, ikijumuisha VAT. 
Pamoja na chaneli mpya ya Azam Sports HD, malipo hayo yatajumujisha chaneli za klabu za Manchester United, Liverpool na Real Madrid  ambazo kwa sasa ni sehemu ya kifurushi cha  Azam Play. 
Kadhalika malipo ya mwezi kwa kifurushi cha Play kitapunguzwa hadi Tsh25,000 kuanzia sasa. Kwa wale wasiokuwa na luninga zenye uwezo wa kuona picha za HD au waya maalum wa HD (HDMI), watapata chaneli mpya na kufuatilia La Liga na mengineyo – japo si kwa ubora wa HD.  
Pia kwa wateja wasiohitaji kujiunga na kiufurushi kipya hawapaswi kuwa na wasiwasi wa kutoona michezo ya VPL kwani itaendelea kuoneshwa kupitia  Azam One na Azam Two kama ilivyokuwa kabla – Jambo lililo tofauti ni kuwa michezo yenye mvuto zaidi itaoneshwa pia kwenye Azam Sports HD.
Zaidi ya La Liga na VPL, Azam Sports HD itakuwa na vipindi mbalimbali vya kimichezo  vitakavyojumuisha michezo ya Ligi za soka za Uganda, Kenya na, Burundi – itakayoanza hivi karibuni.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington amesema “Uzinduzi wa Azam Sports HD ni hatua kubwa katika maendeleo ya AzamTV. 
Mwenyeki wa klabu ya Azam FC, Sheikh Said Muhammad alikuwepo


Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC, Said Tuliy kulia na Collin Frisch kushoto

Hata kabla ya ya kuanza mwaka 2013 tulijipanga kukidhi mahitaji ya teknolojia kwa ajili ya kutoa picha za ubora wa  HD ili kutuwezesha baadaye kumpatia mtazamaji picha bora zaidi bila kulazimika kununua vifaa vipya. Jambo ambalo hatukulitazamia ni kutekeleza hilo ndani ya muda mfupi – na kuanzisha chaneli  kwa kuonesha moja kwa moja soka la La Liga! Ambalo ni bora zaidi barani Ulaya. Uwezo wa kuona moja kwa moja na katika HD timu mzipendazo huko Hispania na kwa VPL, pamoja na vipindi vingine vya michezo kutoka sehemu mablimbali duniani, unatoa chaguo muhimu na ambalo wateja wetu wanalimudu. Huu ni mwanzo tu – jiandae kwa makubwa zaidi” 



Mourinho:Daktari'mjinga' hatakuwepo uwanjani


Dakta Eva Carneiro amehudumu Stamford bridge kwa miaka 5 sasa

Meneja wa Chelsea manager Jose Mourinho amekariri msimamo wake dhidi ya kitengo cha utabibu cha timu yake.
Mourinho aliwakaripia Dakta Eva Carneiro na Jon Fearn kwa kuingia uwanjani huku timu hiyo ikisalia na wachezaji wachache kufuatia kufurushwa kwa kipa nambari moja Thibaut Courtois katika mechi ngumu ya kufungua msimu kati yao na Swansea .

Bi Carneiro aliingia uwanjani katika muda wa lala salama kumtibu kiungo wa Chelsea Eden Hazard

Bi Carneiro aliingia uwanjani katika muda wa lala salama kumtibu kiungo wa Chelsea Eden Hazard ambaye alionekana kagongwa kifundo cha mguu.
'The special one' alisema kuwa daktari mkuu Carneiro na msaidizi wake Fearn hawatakuwa uwanjani Chelsea itakapokuwa ikipambana na Manchester City siku ya jumapili.

Carneiro aliwakilishwa katika mkutano huo na mawakili wake kutoka kwa kampuni ya mawakili ya Mishcon de Reya.

''Hii haimaanishi kuwa hawatakuwepo siku nyingine ,katika siku za usoni'' alisema Mourinho.
Kocha huyo aliyasema hayo baada ya kukutana na kitengo kizima cha utabibu cha Chelsea siku ya Alhamisi.
Carneiro aliwakilishwa katika mkutano huo na mawakili wake kutoka kwa kampuni ya mawakili ya Mishcon de Reya.

Mourinho amekariri kuwa Daktari 'mjinga' hatakuwepo uwanjani

Mourinho aliwataja Carneiro na Fearn kuwa 'wajinga' baada yao kuingia uwanjani kumtibu Hazard katika dakika za lala salama ya mechi ya kufungua msimu.
Kutokana na shinikizo la wapinzani wao Mourinho aliona kuwa kumuondoa Hazard katika kipindi hicho kuliwasaidia wapinzani wao kuwa na wachezaji wawili zaidi hivyo kuwazidi nguvu.

Mourinho alisema hajuti kuwaita ''wajinga''

Mourinho alipoulizwa iwapo anauhusiano mzuri na na kitengo hicho cha utabibu alisema kuwa
''Mimi nao tunahusiana kama kawaida tu vile ''

Mourinho amesema kuwa uhusiano wao ni wa wazi na kuwa haoni kosa la matamshi yake

'Wenyewe wamenieleza kuwa hawajawahi kushabikiwa zaidi ya kipindi hichi nilipoingia Chelsea''
''Walinieleza kuwa wanahitaji kukosolewa ili na wao wajiendeleze''

Kombe la dunia:Timu 3 za Afrika zashindwa



Uganda ililazwa na New Zealand

Timu tatu kutoka Afrika ziliambulia kichapo katika kombe la dunia la mpira wa pete inayoendelea Sydney Australia.
Wawakilishi wa Afrika Mashariki ,Uganda, waliambulia kibano cha alama 76-33 mikononi mwa New Zealand katika hatua ya nusu fainali huko Sydney.
Kufuatia kushindwa huko Uganda sasa inajiunga na Afrika Kusini na Malawi ambazo pia hazikuwa na siku nzuri.
Afrika kusini ilikuwa imechapwa alama 62-46na Uingereza.

Afrika kusini ilikuwa imechapwa alama 62-46na Uingereza.

Malawi kwa upande wake itajilaumu yenyewe kwa kuboronga katika muda wa lala salama wa mechi hiyo baada ya kushindwa na Jamaica kwa alama moja pekee.
Malawi ilikuwa uongozini hadi dakika ya mwisho safu ya ulinzi ilipozembea na kuiruhusu Jamaica kufunga bao la kusawazisha na kisha kuwapiku.
Kufuatia kichapo hicho cha alama moja Malawi walishindwa kufuzu kwa mkumbo wa nusu fainali ya mashindano hayo.

Mataifa hayo ya Afrika yamesalia kuwania nafasi ya 5 hadi 16.

Mkufunzi wa Malawi Mary Waya ameiambia BBC michezo kuwa timu yake ndiyo iliyokuwa bora ila ilikosea tu ilipowadia wakati wa kuwa wakakamavu kisaikolojia.
Kufuatia matokeo hayo sasa Mataifa hayo ya Afrika yamesalia kuwania nafasi ya 5 hadi 16.
Mashindano hayo yanaendelea.

Hakuna maoni: