KIPORO CHA YANGA NA MTIBWA CHARUDISHWA KWENYE JOKOFU!!!!!
SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limekubali kuisogeza mbele mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya mabingwa watetezi, Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar iliokuwa ichezwe Jumatano (Aprili 6, 2016) na badala yake itapigwa Aprili 16 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hiyo inafuatia malalamiko ya Yanga kupangiwa mechi tatu ndani ya wiki moja kabla ya kumenyana na Al Ahly ya Misri Jumamosi ijayo katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Hiyo inafuatia malalamiko ya Yanga kupangiwa mechi tatu ndani ya wiki moja kabla ya kumenyana na Al Ahly ya Misri Jumamosi ijayo katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Maana yake, Yanga SC watashuka dimbani leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na Kagera Sugar ya Bukoba katika mfululizo wa Ligi Kuu na baada ya hapo watakwenda kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Al Ahly mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Murro amesema kwamba mechi hiyo imeondolewa na badala yake itachezwa Aprili 16, kama ilivyopangiwa na Shirikisho hilo.
Alisema kwa matokeo hayo, kikosi hicho baada ya mchezo wa leo dhidi ya Kagera Sugar, wataendelea kujifua kujiandaa na mechi dhidi ya Al Ahly iliyopangwa kufanyika Aprili 9 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi amesema wao wamekataa kuahirishiwa mchezo wao na Ndanda FC na watashuka dimbani Aprili 6 kumalizia kiporo hicho.

![]() |
Kikosi cha Yanga kilichomenyana na Al Ahly mwaka 2014 |
TIMU ya taifa ya Vijana ya umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys imeibuka kidedea baada ya kuifunga ile ya Misri Mapharao mabao 2-1, katika mechi ya kirafiki ya kujipima nguvu kujiandaa na michuano ya kufuzu fainali ya vijana ya mataifa ya Afrika.
Mechi hiyo iliokuwa ikichezeshwa na mwamuzi wa mwenye beji ya FIFA Israel Nkongo Serengeti Boys ilianza kupata bao dakika ya 15,kupitia mchezaji Benedicto aliyeachia shuti kali baada ya kuwatoka mabeki na wa timu hiyo na mpira kutinga wavuni.

Zikiendelea kushambuliana kwa kasi timu hizo huku Serengeti Boys ikimiliki mpira kwa asilimia 51, wakati Misri walimiliki kwa asilimia 49 hadi timu hizo zinakwenda mapunziko Serengeti Boys ilikuwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi sana huku Misri ikionyesha kutafuta bao la kusawazisha kutokana na wachezaji wake kucheza kwa kasi, iliowafanya mabeki wa Serengeti kujichanganya na mshambuliaji Diah Waheed kupachika bao la kusawazisha dakika 85.
Bao hilo liliamsha mashambulizi kwa Serengeti boys,ambao walikosa bao la pili dakika chache baada ya lile la Misri,lakini hawakukata tamaa kuendelea kutafuta pointi tatu wakiwa katika uwanja wa nyumbani.
Iliwachukua dakika ya 90, Serengeti kusawazisha bao lililofungwa na Ally Husein dakika ya 90 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18, lililomwacha kipa wa Mafarao pembeni na kutinga wavuni. Serengeti Boys watarudiana Jumanne hapa Dar es Salaam.
YANGA SC itamkosa kiungo wake, Haruna Niyonzima leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Nahodha huyo wa Rwanda anasumbuliwa na Malaria, hivyo hatakuwemo kabisa kwenye programu ya mechi mbili zijazo za Yanga.
Baada ya mechi na Kagera Sugar leo , Yanga watarudi dimbani kwenye Uwanja huo huo Jumamosi ijayo kumenyana na Al Ahly ya Misri katika Ligi ya Mabingwa ya Afrika.

Na Niyonzima hatacheza mechi dhidi ya Ahly kwa sababu atakuwa anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano alizopewa kwenye mechi mfululizo za Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya APR ya kwao, Rwanda.
Pamoja na kumkosa kiungo wa Amavubi leo, habari njema ni kwamba Nahodha wa timu, beki Nadir Haroub 'Cannavaro' sasa yuko fiti kabisa kurejea uwanjani.
Cannavaro alicheza kwa dakika tano za mwisho katika mchezo dhidi ya Ndanda FC Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alhamisi Yanga ikishinda 2-1 baada ya kukosekana tangu Novemba mwaka jana alipoumia akiichezea timu ya taifa dhidi ya Algeria mjini Blida.
Mbwana Samatta akishangilia baada ya kufunga katika ushindi wa 4-1 dhidi ya KV Oostende kwenye mchezo uliopita wa KRC Genk
Na Nahodha huyo wa Tanzania alifanya kazi nzuri kwa kuifungia timu yake bao pekee kwenye ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji Chad mjini D’jamena wiki iliyopita.
Hata hivyo, bahati mbaya ilikuwa ni kazi bure baada ya matokeo hayo kufutwa kufuatia Chad kujitoa na kusababisha hadi mechi ya marudiano isichezwe.
Mchezo wa leo dhidi ya moja ya timu maarufu nchini Ubelgiji, RSC Anderlecht utakuwa wa saba kwa Samatta tangu ajiunge na Genk Januari mwaka huu akitokea TP Mazembe ya DRC, akiwa amefunga jumla ya mabao mawili. Kabla ya kufunga katika ushindi wa 4-1 dhidi ya KV Oostende, Samatta pia alifunga katika ushindi wa 3-2 baada ya kuingia dakika 15 za mwisho dhidi ya Club Brugge.
Mechi nyingine alizocheza Samatta tangu atue Genk, zote akitokea benchi dakika za mwishoni ni dhidi ya Standard Liege (Genk) wakifungwa 2-1, dhidi ya Lokeren wakitoa sare ya 0-0, dhidi ya Waasland-Beveren wakishinda 6-1 na dhidi ya Mouscron-Peruwelz wakishinda 1-0 pia ugenini.
source bin zubery
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni