Baada ya kuchapwa mechi zake zote tatu na
kutolewa mapema, timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasii salama leo
alfajiri ikitokea nchini Afrika Kusini ilipokua ikishiriki michuano ya Kombe la
Cosafa, huku kocha Mart Nooij akisema amestaajabu.
Stars ambayo jana jioni ilipoteza mchezo wake
wa mwisho dhidi ya Lesotho baada ya kufungwa bao 1 - 0, imerejea baadaa ya
kupoteza michezo yote mitatu ya kundi B, baada ya kufungwa na Swaziland,
Madagascar na Lesotho.
Mara baada ya mchezo wa jana dhidi ya Lesotho,
kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij alisema amesikitishwa na matokeo ya timu
yake katika hatua hiyo ya awali baada ya kupoteza michezo yote mitatu.
Nooij alisema, mpira wa miguu umebadilika
kwani matarajio yake yamekua tofauti, kwani kiwango walivyoonyesha wapinzani
wake katika kundi B vimemstajaabisha.
“Mpira wa sasa hautazami nani yupo juu katika
renki za FIFA, tulikua na matarajio ya kufanya vizuri katika michuano hii
lakini baada ya dakika ya 90 za kila mchezo matokeo hayakua mazuri kwetu”
alisema Nooij”
Kuhusu kufuzu kwa AFCON 2017, Nooij amesema
katika kikosi chake alichokwenda nacho Cosafa alikua na wachezaji saba
aliowapandisha, anaamini wamepata uzoefu, na sasa atawajumuisha na wachezaji
ambao hawakuweza kushiriki michuano hiyo kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.
Taifa Stars inatarajia kucheza kucheza mchezo wake wa kwanza wa
kuwania kufuzu kwa AFCON 2017 dhidi ya Misri, tarehe 14 Juni 2015 katika uwanja
wa Borg el Arab jijini Alexandria.
Kuhusu kufuzu kwa
AFCON 2017, Nooij amesema katika kikosi chake alichokwenda nacho Cosafa alikua
na wachezaji saba aliowapandisha, anaamini wamepata uzoefu, na sasa
atawajumuisha na wachezaji ambao hawakuweza kushiriki michuano hiyo kujiandaa
na mchezo dhidi ya Misri.
Taifa Stars inatarajia
kucheza kucheza mchezo wake wa kwanza wa kuwania kufuzu kwa AFCON 2017 dhidi ya
Misri, tarehe 14 Juni 2015 katika uwanja wa Borg el Arab jijini Alexandria.
IMETOLEWA NA
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
KUHUSU MKATABA NA STARS
Mholanzi huyo ataendelea na kazi kwa hoja moja tu ya msingi,
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) halina fedha za kumlipa kuvunja naye Mkataba,
ambao unamalizika Mei mwakani.
Kamati ya Utendaji ya TFF itakutana kesho Dar es Salaam kujadili
mwenendo wa timu zote za taifa na ajenda kubwa inatarajiwa kuwa Nooij, ambaye
katika mechi 16 alizoiongoza Stars tangu awasili mwishoni mwa Aprili kuchukua
mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen ameshinda tatu tu, akifungwa sita na sare sita.
Stars imefungwa mechi zote tatu za COSAFA 1-0 na Lesotho jana 2-0
na Madagascar Jumatano na 1-0 na Swaziland Jumatatu.
TFF ilihadaika na wasifu mzuri wa Nooij aliyetua Tanzania akitokea
klabu ya St George ya Ethiopia Aprili mwaka jana na kumpa Mkataba mnono.
Wasifu wa Nooij unasema amewahi kuwa mwalimu maalum katika
programu za maendeleo ya soka katika Chama cha Soka Uholanzi (DFA) na pia
amewahi kufundisha timu ya EVC 1913 ya Marekani na baadaye Kazakhstan.
Alikuwa kocha wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20
ya Burkina Faso katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2003 na mwaka 2004
alikuwa kocha wa muda wa klabu ya FC Volendam ya Uholanzi.
Mwaka 2007 aliteuliwa kuwa kocha wa Msumbiji na akaiwezesha kufuzu
kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2010, hiyo ikiwa ni mara ya
kwanza Mambas wanashiriki AFCON baada ya msoto wa miaka 12.
Hata hivyo, katika fainali hizo, Msumbiji ilishika mkia katika
kundi lake baada ya kuambulia sare moja na kufungwa mechi mbili. Baada ya
kukosa tiketi ya AFCON 2012, Nooij akajiuzulu Septemba mwaka 2011 na nafasi
yake kuchukuliwa na Mjerumani, Gert Engels.
Aprili 19 mwaka 2012, aliajiriwa na klabu ya Santos ya Afrika
Kusini, ambako hata hivyo alifukuzwa Desemba 18, mwaka 2012 na kuhamia St
George ya Ethiopia kabla ya kuja Tanzania Aprili mwaka jana.
Nooij sasa ataiongoza Stars katika mechi za kufuzu AFCON ikianza
na Msiri Juni 13 wakati Julai itakuwa mchezo wa kufuzu CHAN dhidi ya Uganda.
MADAGASCAR imetinga robo fainali ya Cosafa
baada ya kufanikiwa kumaliza vinara wa kundi B wakiipiku Swaziland kwa idadi
nzuri ya magoli ya kufunga na kufungwa.
Timu hizo ambazo zilizokuwa zinachuana kusaka
timu moja ya kutinga robo fainali zimetoka sare ya 1-1 usiku huu.
Mechi ya kwanza ya kundi hilo, Madagascar
walishinda 2-1 dhidi ya Lesotho, mechi ya pili wakaifumua 2-0 Tanzania ‘Taifa
Stars’ na jana wametoka sare ya 1-1 na Swaziland.
Kwa matokeo hayo Madagascar wamefunga magoli 5
na kufungwa 2.
Kwa upande wa Swaziland wao walianza michuano
kwa kuifunga 1-0 Taifa Stars, wakashinda 2-0 dhidi ya Lesotho na jana wametoka
sare ya 1-1 na Madagascar, hivyo wamefunga magoli 4 na kufungwa 1.
Kwa matokeo hayo, mei 24 mwaka huu Madagascar
watacheza mechi ya robo fainali dhidi ya Ghana uwanja wa Moruleng majira ya saa
9:00 kwa saa za Afrika kusini sawa na saa 10:00 kwa saa za Afrika mashariki.
Mechi nyingine ya robo fainali siku hiyo
itawakutanisha Malawi na Msumbiji.
Kwa upande wa kundi A, Namibia walifuzu robo
fainali na watachuana na Zambia mei 25 mwaka huu uwanja wa Royal Bafokeng
Sports Palace majira ya saa 11:30 kwa saa za Sauzi sawa na saa 12:30 kwa saa za
Tanzania.
Mechi nyingine ya robo fainali siku ya jumatatu
itawakutanisha wenyeji Afrika kusini dhidi ya Botswana.
NDANDA WADAI CHAO
Licha ya kujituma na
kuhakikisha timu yao imebaki katika Ligi Kuu Bara, bado baadhi ya wachezaji wa
Ndanda FC wanadai fedha zao za malimbikizo ya mishahara na zile za usajili.
Wakizungumza kwa
sharti la kutotajwa, wachezaji hao ambao ni mashujaa kwa kuikoa timu hiyo
kuteremka daraja walisema hawaelewi kwa nini hawalipwi fedha zao wakati mara
kadhaa Mbunge wa Mtwara Vijijini na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, amekuwa akitoa
fedha.
Alipotafutwa Ofisa
Habari wa Ndanda, Idrissa Bandari, alisema: “Kweli tunadaiwa ila hatujui
tutawalipa lini hao wachezaji.”
SHERMN ; UKWI MOTO WA KUOTEA MBALI
|
|
Straika wa Yanga, Kpah
Sherman, ameweka unafiki pembeni na kusema nyota wa Simba, Emmanuel Okwi, kwa
jinsi anavyocheza uwanjani, ana uhakika wa kucheza soka popote pale hata nje ya
Afrika.
Sherman, raia wa
Liberia ambaye alitua Yanga Desemba mwaka jana akitokea Klabu ya Cetinkaya ya
Cyprus, amewahi kucheza timu moja na kiungo wa Mtibwa Sugar, Henry Joseph
katika kikosi cha Kongsvinger ya Norway.
Sherman amesema Okwi
anajua majukumu yake uwanjani na kwa uwezo wake, anaweza kucheza soka la
kulipwa popote pale Afrika hata nje ya bara hili.
“Okwi ni rafiki yangu
wa karibu, anacheza kwa kujituma sana, anamiliki mpira, anatumia akili nyingi
sana uwanjani na vitu vingine vingi, ambavyo naweza kusema anaweza kucheza
popote,” alisema Sherman ambaye ameifungia Yanga mabao sita tangu alipojiunga
nayo.
Wakati huohuo, Sherman
alisema pengo la winga Mrisho Ngassa aliyejiunga na Free State kwa dau la dola
150,000 (Sh milioni 300) katika timu yao, linahitaji mtu makini kuliziba,
vinginevyo timu haitakuwa imara.
VURUGU ZA BURUNDI SIMBA NAO NI
WAATHIRIKA
|
Simba imeamua
kumsubiri mshambuliaji Laudit Mavugo amalize mechi mbili katika kikosi chake
cha Vital’O kabla ya kuja kujiunga nayo kwa ajili ya majaribio. |
Lakini vurugu za
kumpinga Rais Pierre Nkurunziza ambaye anataka kugombea kwa muhula wa tatu,
ndizo zimechangia zaidi Simba kufanikisha jambo hilo.
Mwenyekiti wa Kamati
ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ambaye amekuwa akilifuatilia suala
hilo kwa karibu, amekiri vurugu hizo zimechangia kuongeza ugumu wa jambo hilo.
“Kweli hapa kuna suala
la kusubiri amalize ligi na zimebaki mechi mbili. Tumefanya mazungumzo na klabu
yake, pia imani yangu mambo yatakwenda vizuri.
Mavugo amekuwa tegemeo
katika safu ya ushambuliaji wa Vital’O na aliwahi kufanya kazi na Kocha Goran
Kopunovic.
Kopunovic ndiye
aliyempendekeza Mavugo kwa kuwa alikuwa mchezaji wake akiwa Polisi Rwanda.
Lakini mwisho yeye ameondoka baada ya kutaka apewe dau la Sh milioni 100 ili
asaini mkataba mpya, jambo ambalo Simba hawakukubaliana naye.
Simba imekuwa haina
straika wa uhakika wa ‘kucheka’ na nyavu mara baada ya kumruhusu Amissi Tambwe
aondoke.
Tambwe aliondoka Simba
akiwa mchezaji huru, Yanga ikaokota ‘dodo’ na sasa ni kati ya wachezaji
inaowategemea katika ufungaji.
KIMATAIFA
ADEBAYOR APEWA MDA WA
KUSULUHISHA MGOGORO
Mchezajii wa kilabu ya
Tottenham Emmanuel Adebayor amepewa mapumziko kwa mara ya pili msimu huu lakini
hatma yake katika kilabu ya Spurs haijulikani.
Mchezaji huyo wa taifa
la Togo mwenye umri wa miaka 31 ameandika kuhusu matatizo ya famili yake katika
mtandao wa facebook na kusema kuwa alikuwa ameamua kujiuua.
Atakosa mechi ya siku
ya jumapili kati ya kilabu yake na Everton mbali na ziara ya Kuala Lumpur na
baadaye nchini Sidney.
''Tumempa mda wa
kusuluhisha mzozo na familia yake'',alisema kocha wa kilabu hiyo Mauricio
Pochettino.Ni miasha yakje ya kibinafsi .Niliongea naye mapema wiki hii,ni hali
ngumu kwake''.
Adebayor alijiunga na
klabu ya Spurs mwaka 2011 kutoka Manchester City kupitia mkopo kabla ya mabao
18 aliyofunga akiwa na Hotspurs kumwezesha kupewa kandarasi ya kudumu.
Kocha msaidizi wa Manchester United Ryan Giggs
amesema ni kituko kwa Manchester United kushangilia nafasi ya nne.
Giggs ambaye ameichezea United kwa miaka 27,
ameshinda mara 13 taji la Premier League na mataji mawili ya Champions League
kama mchezaji.
Baada ya kudondoka kwa timu chini ya David
Moyes, hatimaye United ikiwa na Louis van Gaal imejitutumua na kushika nafasi
ya nne, jambo linloonekana kama ushindi fulani.
Giggs amekiri kufurahia mafanikio ya Manchester
United katika msimu wake wa kwanza kama msaidizi wa Van Gaal lakini akasema
msimu ujao ni wa kupigania ubingwa.
Akizungumza katika sherehe za kufunga msimu kwa
klabu hiyo ya Old Trafford, Giggs akasema: Inashangaza kwa mtu ambaye umekuwa
kwenye klabu hii kwa muda mrefu na kwa mafanikio ya hali ya juu, kusimama na
kushangilia nafasi ya nne.
“Lakini sio siri na bila hiyana, hiki ndicho
tulichodhamiria wakati msimu uliopokuwa unaanza – kupata nafasi ya kucheza
Champions League. Ila msimu ujao tunataka kupigania mataji”.
Manchester United ina uwezekano wa kushika
nafasi ya tatu kama itashinda mchezo wake wa mwisho Jumapili na wakati huo huo
Arsenal ifungwe.
REAL MADRID
YAWASILIANA NA BENITEZ
Mkufunzi wa kilabu ya
Napoli Rafael Benitez ameorodheshwa miongoni mwa makocha wataokumrithi Carlo
Ancelotti katika kilabu ya Real Madrid.
Ancelotti anatarajiwa
na wengi kuachana na kilabu hiyo baada ya mechi ya mwisho na Getafe wikiendi
hii.
Mazungumzo kati ya
Real Madrid na Benitez yanaendelea huku kandarasi ya Benitez katika kilabu ya
Napoli ikitarajiwa kukamilika mwezi ujao,ijapokuwa hakuna makubaliano
yalioafikiwa.
Klabu ya West Ham pia
iliwasiliana na kocha huyo ambaye aliwahi kuifunza Chelsea na Liverpool.
Mkufunzi wa West Ham
ambaye anaiandaa West Ham dhidi ya Newcastle anatarajiwa kuanzisha mazungumzo
na klabu hiyo kuhusu hatma yake wiki ijayo.
Benitez alianza kazi
ya ukufunzi katika kilabu ya Real Madrid B na pia amewahi kuifunza Valladolid,Osasuna,Etramadura,TenerifeValencia
na Inter Milan.
Wakati tetesi za Carlo Ancelotti kuwa kikaangoni
Santiago Bernabeu zikizidi kusambaa, wakala wa Rafael Benitez amefichua kuwa
mteja wake atafurahia nafasi ya kuikochi Real Madrid.
Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, kocha
huyo wa Napoli hana mpango wa kusaini mkataba mpya kwa miamba hiyo ya Serie A
huku habari zikisema ni mmoja wa makocha wanaowaniwa na Real Madrid
kuziba nafasi ya Carlo Ancelotti.
Kama vile hiyo haitoshi, inasemekana mmiliki wa
AC Milan Silvio Berlusconi naye anamtaka Carlo Ancelotti arejee nyumbani
kuikochi timu hiyo.
Benitez amewahi kuhusishwa na Real Madrid mara
kadhaa huko nyuma hasa baada ya kuipa Valencia mataji mawili ya La Liga na pale
alipoiwezesha Liverpool kutwaa kombe la Champions League.
Akiongea na kituo cha TV cha Cuatro, wakala wa
Benitez, Manuel García Quilón alisema: “Huu ni uvumi wa nguvu sana, hakuna
maongezi yoyote mpaka muda huu, lakini mteja wangu atafurahia nafasi hiyo.
“Rafa alikuwa mchezaji wa Real Madrid, akawa
kocha wa vijana klabuni hapo na anatokea Madrid – ni nani ambaye hatafurahishwa
na nafasi hiyo?
“Sipo ndani ya kichwa chake, lakini najaribu
kuvuta picha na kuona ni jinsi gani atafurahia mafasi hiyo”.
Bosi wa Napoli Rafa Benitez anatarajiwa kuanza maongezi
na rais wa Real Madrid, Florentino Perez kwaajili ya kurejea Santiago
Bernabeu
Manchester City inatajwa kuwa iko kwenye
nafasi nzuri zaidi ya kumtwaa Raheem Sterling wa Liverpool pindi dirisha la
usajili litakapo funguliwa mwezi ujao.
City ipo tayari kulipa pauni milioni 45
kwa winga huyo wa kimataifa wa England sambamba na mshahara wa pauni
120,000 kwa wiki.
Hata hivyo kocha wa City Manuel Pellegrini
amesema kwa sasa hawezi kuongea chochote kuhusu Sterling: “Sijui nini kitatokea
kwa Raheem, kuna wachezaji wengi muhimu ambao kila klabu ingependa kuwa nao.
“Tunamaliza msimu kesho na baada ya hapo
tutaangalia ni wachezaji gani wa kuwaleta klabuni kwetu.
“Hakutakuwa na mabadiliko makubwa sana kwa
sababu sidhani kama tunahitaji kufanya hivyo. Tutajitahidi kuwa na kikosi imara
kila mwaka, sio kwasababu tumekosa taji msimu huu, bali ni kwasababu ni muhimu
kufanya mabadiliko yenye tija kila mwaka.”
Kama wanasheria wa Barcelona watafanikiwa
kutengua adhabu ya klabu kufungiwa usajili, basi biashara ya kwanza itakuwa ni
kwa kiungo wa Arsenal, Aaron Ramsey (pichani juu kulia).
Barcelona inataka kumnunua Ramsey – Arsenal
inaweza kuwa chimbo la kuineemesha Barcelona kwa mara nyingine tena.
Pauni milioni 50 zinatajwa kuwa ndio kiasi
kinachoandaliwa na Barcelona kwaajili ya nyota huyo kimataifa wa Wales,
wakitaraji kumchukua mchezaji wa tisa kutoka Arsenal kuanzia mwaka 2000.
Barcelona wapo kwenye kifungo cha kusajili
lakini wana matumaini ya kuachiwa huru katika dirisha la kiangazi na iwapo kama
hilo halitafanikiwa basi watakomaa na Ramsey katika dirisha la Januari pale
adhabu yao itakapokuwa imeisha.