Jumamosi, 23 Mei 2015

MAJIDI NA HAMADI DIMBA MAY 23 2015


Baada ya kuchapwa mechi zake zote tatu na kutolewa mapema, timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasii salama leo alfajiri ikitokea nchini Afrika Kusini ilipokua ikishiriki michuano ya Kombe la Cosafa,  huku kocha Mart Nooij  akisema amestaajabu.

Stars ambayo jana jioni ilipoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Lesotho baada ya kufungwa bao 1 - 0, imerejea baadaa ya kupoteza michezo yote mitatu ya kundi B, baada ya kufungwa na Swaziland, Madagascar na Lesotho. 

Mara baada ya mchezo wa jana dhidi ya Lesotho, kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij alisema amesikitishwa na matokeo ya timu yake katika hatua hiyo ya awali baada ya kupoteza michezo yote mitatu.
Nooij alisema, mpira wa miguu umebadilika kwani matarajio yake yamekua tofauti, kwani kiwango walivyoonyesha wapinzani wake katika kundi B vimemstajaabisha.
“Mpira wa sasa hautazami nani yupo juu katika renki za FIFA, tulikua na matarajio ya kufanya vizuri katika michuano hii lakini baada ya dakika ya 90 za kila mchezo matokeo hayakua mazuri kwetu” alisema Nooij” 
Kuhusu kufuzu kwa AFCON 2017, Nooij amesema katika kikosi chake alichokwenda nacho Cosafa alikua na wachezaji saba aliowapandisha, anaamini wamepata uzoefu, na sasa atawajumuisha na wachezaji ambao hawakuweza kushiriki michuano hiyo kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.

Taifa Stars inatarajia kucheza kucheza mchezo wake wa kwanza wa kuwania kufuzu kwa AFCON 2017 dhidi ya Misri, tarehe 14 Juni 2015 katika uwanja wa Borg el Arab jijini Alexandria.

Kuhusu kufuzu kwa AFCON 2017, Nooij amesema katika kikosi chake alichokwenda nacho Cosafa alikua na wachezaji saba aliowapandisha, anaamini wamepata uzoefu, na sasa atawajumuisha na wachezaji ambao hawakuweza kushiriki michuano hiyo kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.

Taifa Stars inatarajia kucheza kucheza mchezo wake wa kwanza wa kuwania kufuzu kwa AFCON 2017 dhidi ya Misri, tarehe 14 Juni 2015 katika uwanja wa Borg el Arab jijini Alexandria.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)



KUHUSU MKATABA NA STARS
Mholanzi huyo ataendelea na kazi kwa hoja moja tu ya msingi, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) halina fedha za kumlipa kuvunja naye Mkataba, ambao unamalizika Mei mwakani. 

Kamati ya Utendaji ya TFF itakutana kesho Dar es Salaam kujadili mwenendo wa timu zote za taifa na ajenda kubwa inatarajiwa kuwa Nooij, ambaye katika mechi 16 alizoiongoza Stars tangu awasili mwishoni mwa Aprili kuchukua mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen ameshinda tatu tu, akifungwa sita na sare sita.

Stars imefungwa mechi zote tatu za COSAFA 1-0 na Lesotho jana 2-0 na Madagascar Jumatano na 1-0 na Swaziland Jumatatu.
TFF ilihadaika na wasifu mzuri wa Nooij aliyetua Tanzania akitokea klabu ya St George ya Ethiopia Aprili mwaka jana na kumpa Mkataba mnono. 
Wasifu wa Nooij unasema amewahi kuwa mwalimu maalum katika programu za maendeleo ya soka katika Chama cha Soka Uholanzi (DFA) na pia amewahi kufundisha timu ya EVC 1913 ya Marekani na baadaye Kazakhstan.
Alikuwa kocha wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Burkina Faso katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2003 na mwaka 2004 alikuwa kocha wa muda wa klabu ya FC Volendam ya Uholanzi.
Mwaka 2007 aliteuliwa kuwa kocha wa Msumbiji na akaiwezesha kufuzu kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2010, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza Mambas wanashiriki AFCON baada ya msoto wa miaka 12. 
Hata hivyo, katika fainali hizo, Msumbiji ilishika mkia katika kundi lake baada ya kuambulia sare moja na kufungwa mechi mbili. Baada ya kukosa tiketi ya AFCON 2012, Nooij akajiuzulu Septemba mwaka 2011 na nafasi yake kuchukuliwa na Mjerumani, Gert Engels.
Aprili 19 mwaka 2012, aliajiriwa na klabu ya Santos ya Afrika Kusini, ambako hata hivyo alifukuzwa Desemba 18, mwaka 2012 na kuhamia St George ya Ethiopia kabla ya kuja Tanzania Aprili mwaka jana. 
Nooij sasa ataiongoza Stars katika mechi za kufuzu AFCON ikianza na Msiri Juni 13 wakati Julai itakuwa mchezo wa kufuzu CHAN dhidi ya Uganda.


 

 

WABABE WA STARS WATINGA ROBO FAINALI COSAFA, SASA USO KWA USO NA GHANA


MADAGASCAR imetinga robo fainali ya Cosafa baada ya kufanikiwa kumaliza vinara wa kundi B wakiipiku Swaziland kwa idadi nzuri ya magoli ya kufunga na kufungwa.
Timu hizo ambazo zilizokuwa zinachuana kusaka timu moja ya kutinga robo fainali zimetoka sare ya 1-1 usiku huu.
Mechi ya kwanza ya kundi hilo, Madagascar walishinda 2-1 dhidi ya Lesotho, mechi ya pili wakaifumua 2-0 Tanzania ‘Taifa Stars’ na jana wametoka sare ya 1-1 na Swaziland.
Kwa matokeo hayo Madagascar wamefunga magoli 5 na kufungwa 2.
Kwa upande wa Swaziland wao walianza michuano kwa kuifunga 1-0 Taifa Stars, wakashinda 2-0 dhidi ya Lesotho na jana wametoka sare ya 1-1 na Madagascar, hivyo wamefunga magoli 4 na kufungwa 1.
Kwa matokeo hayo, mei 24 mwaka huu Madagascar watacheza mechi ya robo fainali dhidi ya Ghana uwanja wa Moruleng majira ya saa 9:00 kwa saa za Afrika kusini sawa na saa 10:00 kwa saa za Afrika mashariki.
Mechi nyingine ya robo fainali siku hiyo itawakutanisha Malawi na Msumbiji.
Kwa upande wa kundi A, Namibia walifuzu robo fainali na watachuana na Zambia mei 25 mwaka huu uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace majira ya saa 11:30 kwa saa za Sauzi sawa na saa 12:30 kwa saa za Tanzania.
Mechi nyingine ya robo fainali siku ya jumatatu itawakutanisha wenyeji Afrika kusini dhidi ya Botswana.

 

 

NDANDA WADAI CHAO

Licha ya kujituma na kuhakikisha timu yao imebaki katika Ligi Kuu Bara, bado baadhi ya wachezaji wa Ndanda FC wanadai fedha zao za malimbikizo ya mishahara na zile za usajili.


Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa, wachezaji hao ambao ni mashujaa kwa kuikoa timu hiyo kuteremka daraja walisema hawaelewi kwa nini hawalipwi fedha zao wakati mara kadhaa Mbunge wa Mtwara Vijijini na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, amekuwa akitoa fedha.


Alipotafutwa Ofisa Habari wa Ndanda, Idrissa Bandari, alisema: “Kweli tunadaiwa ila hatujui tutawalipa lini hao wachezaji.”

SHERMN ; UKWI MOTO WA KUOTEA MBALI
Straika wa Yanga, Kpah Sherman, ameweka unafiki pembeni na kusema nyota wa Simba, Emmanuel Okwi, kwa jinsi anavyocheza uwanjani, ana uhakika wa kucheza soka popote pale hata nje ya Afrika.

Sherman, raia wa Liberia ambaye alitua Yanga Desemba mwaka jana akitokea Klabu ya Cetinkaya ya Cyprus, amewahi kucheza timu moja na kiungo wa Mtibwa Sugar, Henry Joseph katika kikosi cha Kongsvinger ya Norway.

Sherman amesema Okwi anajua majukumu yake uwanjani na kwa uwezo wake, anaweza kucheza soka la kulipwa popote pale Afrika hata nje ya bara hili.


“Okwi ni rafiki yangu wa karibu, anacheza kwa kujituma sana, anamiliki mpira, anatumia akili nyingi sana uwanjani na vitu vingine vingi, ambavyo naweza kusema anaweza kucheza popote,” alisema Sherman ambaye ameifungia Yanga mabao sita tangu alipojiunga nayo.


Wakati huohuo, Sherman alisema pengo la winga Mrisho Ngassa aliyejiunga na Free State kwa dau la dola 150,000 (Sh milioni 300) katika timu yao, linahitaji mtu makini kuliziba, vinginevyo timu haitakuwa imara.



VURUGU ZA BURUNDI SIMBA NAO NI WAATHIRIKA

  

Simba imeamua kumsubiri mshambuliaji Laudit Mavugo amalize mechi mbili katika kikosi chake cha Vital’O kabla ya kuja kujiunga nayo kwa ajili ya majaribio.


Lakini vurugu za kumpinga Rais Pierre Nkurunziza ambaye anataka kugombea kwa muhula wa tatu, ndizo zimechangia zaidi Simba kufanikisha jambo hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ambaye amekuwa akilifuatilia suala hilo kwa karibu, amekiri vurugu hizo zimechangia kuongeza ugumu wa jambo hilo.

“Kweli hapa kuna suala la kusubiri amalize ligi na zimebaki mechi mbili. Tumefanya mazungumzo na klabu yake, pia imani yangu mambo yatakwenda vizuri.

Mavugo amekuwa tegemeo katika safu ya ushambuliaji wa Vital’O na aliwahi kufanya kazi na Kocha Goran Kopunovic.

Kopunovic ndiye aliyempendekeza Mavugo kwa kuwa alikuwa mchezaji wake akiwa Polisi Rwanda. Lakini mwisho yeye ameondoka baada ya kutaka apewe dau la Sh milioni 100 ili asaini mkataba mpya, jambo ambalo Simba hawakukubaliana naye.

Simba imekuwa haina straika wa uhakika wa ‘kucheka’ na nyavu mara baada ya kumruhusu Amissi Tambwe aondoke.

Tambwe aliondoka Simba akiwa mchezaji huru, Yanga ikaokota ‘dodo’ na sasa ni kati ya wachezaji inaowategemea katika ufungaji.


KIMATAIFA

ADEBAYOR APEWA MDA WA KUSULUHISHA MGOGORO
Mchezajii wa kilabu ya Tottenham Emmanuel Adebayor amepewa mapumziko kwa mara ya pili msimu huu lakini hatma yake katika kilabu ya Spurs haijulikani.
Mchezaji huyo wa taifa la Togo mwenye umri wa miaka 31 ameandika kuhusu matatizo ya famili yake katika mtandao wa facebook na kusema kuwa alikuwa ameamua kujiuua.
Atakosa mechi ya siku ya jumapili kati ya kilabu yake na Everton mbali na ziara ya Kuala Lumpur na baadaye nchini Sidney.
''Tumempa mda wa kusuluhisha mzozo na familia yake'',alisema kocha wa kilabu hiyo Mauricio Pochettino.Ni miasha yakje ya kibinafsi .Niliongea naye mapema wiki hii,ni hali ngumu kwake''.
Adebayor alijiunga na klabu ya Spurs mwaka 2011 kutoka Manchester City kupitia mkopo kabla ya mabao 18 aliyofunga akiwa na Hotspurs kumwezesha kupewa kandarasi ya kudumu.



Kocha msaidizi wa Manchester United Ryan Giggs amesema ni kituko kwa Manchester United kushangilia nafasi ya nne.
Giggs ambaye ameichezea United kwa miaka 27, ameshinda mara 13 taji la Premier League na mataji mawili ya Champions League kama mchezaji.
Baada ya kudondoka kwa timu chini ya David Moyes, hatimaye United ikiwa na Louis van Gaal imejitutumua na kushika nafasi ya nne, jambo linloonekana kama ushindi fulani.
Giggs amekiri kufurahia mafanikio ya Manchester United katika msimu wake wa kwanza kama msaidizi wa Van Gaal lakini akasema msimu ujao ni wa kupigania ubingwa.
Akizungumza katika sherehe za kufunga msimu kwa klabu hiyo ya Old Trafford, Giggs akasema: Inashangaza kwa mtu ambaye umekuwa kwenye klabu hii kwa muda mrefu na kwa mafanikio ya hali ya juu, kusimama na kushangilia nafasi ya nne.
“Lakini sio siri na bila hiyana, hiki ndicho tulichodhamiria wakati msimu uliopokuwa unaanza – kupata nafasi ya kucheza Champions League. Ila msimu ujao tunataka kupigania mataji”.
Manchester United ina uwezekano wa kushika nafasi ya tatu kama itashinda mchezo wake wa mwisho Jumapili na wakati huo huo Arsenal ifungwe.



 REAL MADRID YAWASILIANA NA BENITEZ

Mkufunzi wa kilabu ya Napoli Rafael Benitez ameorodheshwa miongoni mwa makocha wataokumrithi Carlo Ancelotti katika kilabu ya Real Madrid.
Ancelotti anatarajiwa na wengi kuachana na kilabu hiyo baada ya mechi ya mwisho na Getafe wikiendi hii.
Mazungumzo kati ya Real Madrid na Benitez yanaendelea huku kandarasi ya Benitez katika kilabu ya Napoli ikitarajiwa kukamilika mwezi ujao,ijapokuwa hakuna makubaliano yalioafikiwa.
Klabu ya West Ham pia iliwasiliana na kocha huyo ambaye aliwahi kuifunza Chelsea na Liverpool.

Mkufunzi wa West Ham ambaye anaiandaa West Ham dhidi ya Newcastle anatarajiwa kuanzisha mazungumzo na klabu hiyo kuhusu hatma yake wiki ijayo.
Benitez alianza kazi ya ukufunzi katika kilabu ya Real Madrid B na pia amewahi kuifunza Valladolid,Osasuna,Etramadura,TenerifeValencia na Inter Milan.




Wakati tetesi za Carlo Ancelotti kuwa kikaangoni Santiago Bernabeu zikizidi kusambaa, wakala wa Rafael Benitez amefichua kuwa mteja wake atafurahia nafasi ya kuikochi Real Madrid.

Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, kocha huyo wa Napoli hana mpango wa kusaini mkataba mpya kwa miamba hiyo ya Serie A huku habari zikisema ni mmoja wa makocha wanaowaniwa na Real  Madrid kuziba nafasi ya Carlo Ancelotti.

Kama vile hiyo haitoshi, inasemekana mmiliki wa AC Milan Silvio Berlusconi naye anamtaka Carlo Ancelotti arejee nyumbani kuikochi timu hiyo.

Benitez amewahi kuhusishwa na Real Madrid mara kadhaa huko nyuma hasa baada ya kuipa Valencia mataji mawili ya La Liga na pale alipoiwezesha Liverpool kutwaa kombe la Champions League.

Akiongea na kituo cha TV cha Cuatro, wakala wa Benitez, Manuel García Quilón alisema: “Huu ni uvumi wa nguvu sana, hakuna maongezi yoyote mpaka muda huu, lakini mteja wangu atafurahia nafasi hiyo.
“Rafa alikuwa mchezaji wa Real Madrid, akawa kocha wa vijana klabuni hapo na anatokea Madrid – ni nani ambaye hatafurahishwa na nafasi hiyo?

“Sipo ndani ya kichwa chake, lakini najaribu kuvuta picha na kuona ni jinsi gani atafurahia mafasi hiyo”.

Bosi wa Napoli Rafa Benitez anatarajiwa kuanza maongezi na rais wa Real Madrid, Florentino Perez kwaajili ya kurejea Santiago Bernabeu
      



Bottom of Form


Manchester City inatajwa kuwa iko kwenye nafasi nzuri zaidi ya kumtwaa Raheem Sterling wa Liverpool pindi dirisha la usajili litakapo funguliwa mwezi ujao.
City ipo tayari kulipa pauni milioni 45 kwa  winga huyo wa kimataifa wa England sambamba na mshahara wa pauni 120,000 kwa wiki.
Hata hivyo kocha wa City Manuel Pellegrini amesema kwa sasa hawezi kuongea chochote kuhusu Sterling: “Sijui nini kitatokea kwa Raheem, kuna wachezaji wengi muhimu ambao kila klabu ingependa kuwa nao.
“Tunamaliza msimu kesho na baada ya hapo tutaangalia ni wachezaji gani wa kuwaleta klabuni kwetu.
“Hakutakuwa na mabadiliko makubwa sana kwa sababu sidhani kama tunahitaji kufanya hivyo. Tutajitahidi kuwa na kikosi imara kila mwaka, sio kwasababu tumekosa taji msimu huu, bali ni kwasababu ni muhimu kufanya mabadiliko yenye tija kila mwaka.”


Bottom of Form

Kama wanasheria wa Barcelona watafanikiwa kutengua adhabu ya klabu kufungiwa usajili, basi biashara ya kwanza itakuwa ni kwa kiungo wa Arsenal, Aaron Ramsey (pichani juu kulia).
Barcelona inataka kumnunua Ramsey – Arsenal inaweza kuwa chimbo la kuineemesha Barcelona kwa mara nyingine tena.
Pauni milioni 50 zinatajwa kuwa ndio kiasi kinachoandaliwa na Barcelona kwaajili ya nyota huyo kimataifa wa Wales, wakitaraji kumchukua mchezaji wa tisa kutoka Arsenal kuanzia mwaka 2000.
Barcelona wapo kwenye kifungo cha kusajili lakini wana matumaini ya kuachiwa huru katika dirisha la kiangazi na iwapo kama hilo halitafanikiwa basi watakomaa na Ramsey katika dirisha la Januari pale adhabu yao itakapokuwa imeisha.



Hakuna maoni: