Kufuzu AFCON:Taifa Stars yajiandaa
Kocha
Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mdachi Mart Nooij,
amewaita wachezaji 16 kuingia kambini kesho siku ya Jumatano kwa ajili
ya kupimwa afya zao na kujua maandeleo yao kabla ya kuwajumUisha katika
kikosi cha pamoja kitakachokua kwenye maandalizi ya michuano ya kufuzu
ya AFCON 2017 dhidi ya Misri.
Wachezaji walioitwa kuingia kambini
kesho ni, Mohamed Hussein, Peter Manyika, Hassan Isihaka, Jonas Mkude
(Simba SC), Salum Telela, Juma Abdul, Nadir Haroub (Yanga SC), Aishi
Manula, Mudathir Yahya, Frank Domayo, Kelvin Friday (Azam FC), Rashid
Mandawa, Atupele Green (Kagera Sugar), Haroun Chanongo (Stand United)
Malimi Busungu (Mgambo JKT) na Emmanuel Simwanda (African Lyon).
Mara
baada ya kurejea kutoka nchini Afrika Kusini, kocha wa Stars Nooij
aliwapa mapumziko ya siku 10, wachezaji waliokua kwenye michuano ya
Cosafa mpaka Juni Mosi ambapo ndipo watajumuika na wachezaji wengine
waliopo kambini.Tanzania ilifanya vibaya katika michuano hiyo ya Cosafa
na kufungwa nan chi zilizochini katika viwango vya chini vya Fifa,
Swaziland na Madagascar. Kwa mujibu wa msemaji wa Shirikisho la Soka
nchini Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto, ifikapo Juni Mosi, 2015 Taifa
Stars itaanza kambi ya moja kwa moja kujiandaa na mechi dhidi ya Misri
itakayochezwa jijini Alexandria katika uwanja wa Borg El Arab Juni 14,
2015 ikiwajumuisha pia wachezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu
wanaocheza soka la kulipwa katika klabu ya TP Mazembe ya Congo DR. Kabla
ya kuelekea nchini Misri, Taifa Stars inatarajiwa kuweka kambi jijini
Addis Ababa nchini Ethiopia kuanzia tarehe 4,Juni 2015 kwa muda wa wiki
moja kabla ya kuelekea nchini Misri kwenye mchezo huo dhidi ya Mafarao.
Juni 20, 2015 Taifa Stars itawakaribisha Uganda kwenye uwanja wa Aman
mjini Zanzibar katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa
wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika nchini Rwanda 2016, na mchezo
wa marudiano kufanyika baada ya wiki mbili nchini Uganda.
Bolt ashinda mita 200

Mwanariadha
raia wa Jamaica Usain Bolt ameshinda kwa urahis katika shindano lake la
kwanza mwaka huu huko barani Ulaya japokuwa ameshindwa kuvunja rekodi
yake ya sekunde 20, kwenye mbio za mita 200 za Golden Spike huko Ostrava
Jamhuri ya Czech.
Katika shindano hilo lililofanyika jana Bolt
alitumia sekunde 20.13 ikiwa ya rekodi yake ya dunia ya sekunde 19.19
akimbwaga mmarekani Isiah Young "huwezi ridhika kama sivunji sekunde 20"
alisema Bolt ambaye anajiandaa kwa mashindano ya dunia yatakayofanyika
Beijing mwezi August.
Eddie Howe awa meneja bora England
Kocha
wa timu ya soka Bournemouth ya England Eddie Howe ametajwa kuwa meneja
bora wa mwaka wa shirikisho la mameneja wa soka nchini Uingereza LMA.
Kutajwa
kwa meneja huyo kunakuja kufuatia kuiongoza kwa mafanikio klabu yake
ambayo imeingia ligi kuu ya England kwa mara ya kwanza tokea ianzishwe
zaidi ya miaka 100 iliyopita. Howe anakuwa kocha wa pili kutoka nje ya
ligi kuu kushinda tuzo hiyo tangia mwaka 1992. "siamini kabisa, ni
jambao nisilotarajia" alisema kocha huyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni