Alhamisi, 25 Juni 2015

Southgate kuendelea kuwa kocha England


MKUDE NAYE KWA NGASA BONDENI!

Mkude anakwenda kufanya majaribio katika klabu ya Bidvets ya Afrika Kusini.
Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema uongozi umempa ruksa na tayari umezungumza na uongozi wa benchi la ufundi la Taifa Stars.
“Tumemumbeaoa ruhusa Mkude aende kwenye majaribio, kwa kuwa amechaguliwa timu ya taifa, nao tumewasiliana nao.
“Kocha Mkwasa ni kati ya watu ambao wangependa maendeleo ya wachezaji kwenda nje, hii pia itaisaidia Taifa Stars. Hivyo hawezi kuwa na tatizo,” alisema.
Majaribio yanaweza kuwa ya wiki moja hadi zaidi kulingana na mahitaji ya timu hiyo inayomilikiwa na moja ya vyuo vikuu vikongwe barani Afrika cha Wits cha jijini Johannesburg.

MKWASA AOMBA ASIPIGWE MAWE SIMBA

Katika mazungumzo hayo Mkwasa amesema kuna mambo ambayo Watanzania tunapaswa kuyapa nafasi katika Timu ya Taifa.
Kwanza lilikuwa ni lile la kuwapa nafasi vijana wa kikosi chake kwa kuwa ndiyo wanaanza kujipanga.
“Wavumilieni kwa kuwa sasa ndiyo wanajipanga upya tena. Waungeni mkono na msitumie muda mwingi kuwazoemea au kuwapiga.
“Nafikiri hatuko katika hali ambayo tunaweza kusema tumekaa vizuri, tunahitaji kujipanga. Tafadhari tupeni muda,” alisema Mkwasa.
Lakini la pili ni lile ambalo wakati anazungumza, aliwagusa na Simba.
“Nitapita hadi kwenda mazoezi ya baadhi ya timu kwa ajili ya kuangalia wachezaji. Lengo ni kupata wale wenye kiwango chenye msaada.
“Ninaweza kuzungumza na makocha wa timu mbalimbali pia. Mfano naweza kuwatembelea mazoezini na kushauriana nao.
KAIJAGE AWAOMBA WACHEZAJI TANZANITE KURIPOTI KAMBINI KUJIANDAA DHIDI YA ZAMBIA




Timu ya taifa ya soka ya Wanawake 'Tanzanite' wenye umri chini ya miaka 20 (U-20) Tanzanite Stars, imeingia kambini jana jioni Mbande jijini Dar es salaam na itakua ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha wacheaji 22 chini ya Kocha Mkuu, Rogasian Kaijage kinafanya mazoezi asubuhi na jioni katika uwnaja wa Azam uliopo Chamazi kujiandaa na mchezo dhidi ya U-20 ya Zambia utakaofanyika kati ya Julai 10, 11 na 12 jijini Dar es salaam.

Mchezo huo dhidi ya Zambia ni wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Wanawake za Dunia wenye umri chini ya miaka ya 20, zitakazofanyika nchini Papua New Guinea mwaka 2016.

Wachezaji waliopo kambini ni, NajiAati Abbasi, Zuwena Aziz, Shelder Boniface, Stumai Abdallah, Donisia Daniel, Tatu Iddy (Evergreen Queens), Niwael  Khalfani, Maimuna Hamis (Mburahati Queens), Anastazia Anthony, Amisa Athumani, Amina Ramadhani, Neem Paulo (JKT Queens).

Wengine ni Asha Shaban, Rebeka Daniel, Brandina Wincelaus (Tanga), Happines Hezroni, Jane Cloudy (JKT Queens), Wema Richard, Gerwa Lugomba, Sadda Ramadhani (Uzuri Queens), Anna Hebron (Evergreen Queens) na Shehati Mohamed (Mburahati Queens)

Aidha wachezaji Monica Henry, Tumaini Michael (Uzuri Queens), Diana Msewa (Mbeya), na Vailet Nicolaus (Evergreen) bado hawajaripoti kambini wanaombwa kuripoti  na kuungana na wenzao katika maandalizi ya mchezo huo dhidi ya Zambia.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


chanzo saleh jembe

Hakuna maoni: