MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga SC jioni ya leo wamelazimishwa sare ya bila kufungana na SC Villa ya Uganda katika mchezo wa kirafiki, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga SC watajilaumu wenyewe kwa sare hiyo, kwani walipata nafasi kadhaa za kufunga ikiwemo penalti, iliyopaishwa na mchezaji bora wa Ligi Kuu, Simon Msuva dakika za lala salama.
Timu hizo zilianza kushambuliana kwa zamu, huku zote zikicheza soka maridadi ya utulivu na pasi za uhakika kabla ya dakika ya 27 Kasumba Omary wa Villa nusura kumzunguka Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ lakini beki wa kulia Oscar Joshua akaondosha mpira kwenye hatari.
Dakika ya 28 Achema Robert alipiga shuti kali likatoka nje, kabla ya shuti lake lingine kudakwa na kipa wa Yanga SC, Ally Mustafa ‘Barthez’ dakika ya 33.
Malimi Busungu wa Yanga SC alipiga nje dakika ya 32 kufuatia pasi nzuri ya Amisi Tambwe. Busungu tena dakika ya 35 alimdakisha kipa wa Villa, Sebwato Nicolaus baada ya kupiga ndani ya boksi.
Tambwe naye alipoteza nafasi ya kufunga dakika ya 34 baada ya shuti lake kudakwa na kipa wa Villa, Sebweto.
Katika mchezo huo, Kocha mpya wa Simba Dylan Kerr aliingia kuwatazama wapinzani, kipindi cha pili Yanga SC walitengeneza nafasi nzuri, lakini wakashindwa kutumia.
Dakika ya 50 Deus Kaseke aligongesha mwamba, dakika ya 54 krosi nzuri ya Juma Abdul ilidakwa na kipa wa Villa, Sebwato.
Yanga SC ilipata pigo dakika ya 71, baada ya Nahodha wake, Cannavaro kuumia juu ya jicho na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Pato Ngonyani aliyekwenda kucheza vizuri.
Winga mpya machachari wa Yanga SC, Godfrey Mwashiuya aliunganisha vizuri krosi ya Kpah Sherman dakika ya 76, lakini beki wa Villa, Wasibi akaokoa mpira ukiwa unaelekea nyavuni.
Msuva akapaisha penalti dakika ya 78 baada ya kipa wa Villa kumuangusha Kaseke kwenye eneo la hatari na dakika ya 80 Mwashiuya aliipiga shuti maridadi lililookoleea na kipa wa villa kuucheza.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa: Ally Mustaph, Juma Abdul, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Nadir Haroub/Pato Ngonyani dk71, Mbuyu Twite/Andrey Coutinho dk89, Deus Kaseke, Salum Telela, Amis Tambwe/Simon Msuva dk77, Malimi Busungu/Kpah Sherman dk70 na Godfrey Mwashiuya.
MSUVA AWAPA SARE YA 0 - 0 YANGA KWA KUPAISHA PENALTI,
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM

Shirikisho la soka la Ghana GFA limekanusha madai ya ubadhirifu wa fedha katika kombe la dunia la Brazil 2014.
Shirikisho hilo limeitupia tope ripoti ya kamati maalum iliyoundwa kutathmini sababu za matokeo duni huko Brazil 2014.
''Kamati ya Dzamefe'' ilichapisha ripoti yake majuzi na ikaonesha kuwa mpakuaji mipira wa timu ya Black Stars alilipwa kiasi sawa cha fedha na Washambuliaji Asamoah Gyan na hata kocha wa timu ya taifa James Kwesi Appiah.
Meza ya michezo ya BBC ndiyo iliyopasua mbarika kuwa Hamidu alilipwa pesa sawa na kocha na wachezaji nyota .
Ripoti hiyo ilionesha kuwa yule msaidizi anayeokota mipira na kupanga jezi za timu ya taifa alilipwa takriban dola laki moja $100,000.
Ismail Hamidu alipokea pesa hizo japo GFA inailaumu kamati hiyo kwa kuidunisha kazi yake.
Meza ya michezo ya BBC ndiyo iliyopasua mbarika kuwa Hamidu alilipwa pesa sawa na kocha na wachezaji nyota .
Sasa GFA imewataka mawakili wake wawasilishe kesi mahakamani kupinga kuchafuliwa jina
Kamati hiyo vilevile inasema kuwa kunakiasi kikubwa tu cha pesa zilizopewa GFA ambazo hazijabainika zilipo.
Sasa GFA imewataka mawakili wake wawasilishe kesi mahakamani kupinga kuchafuliwa jina.
Ghana ilishindwa kufuzu kwa mkondo wa pili huko Brazil licha ya serikali kutuma zaidi ya dola milioni 3 pesa taslimu kupelekwa Brazil ilikuzima mgomo wa wachezaji waliokuwa wakilalamikia malimbikizi ya marupurupu yao.
Tevez arejea Boca Juniors
Straika wa Argentina Carlos Tevez amekamilisha Uhamisho wake kwenda Boca Juniors kutoka kwa Mabingwa wa Italy Juventus.
Tevez, mwenye Miaka 31, alianzia Soka lake huko kwao na Klabu ya Boca ambayo aliihama Mwaka 2004 kwenda Brazil kuchezea Corinthians na kisha kukaa Miaka 9 akichezea Klabu za Ulaya.
Huko Ulaya alizichezea Klabu za England, West Ham, Mwaka 2006-2007, Manchester United, 2007-2009, na Manchester City, 2009-2013, na kisha kwenda Italy kuichezea Juventus ambako msimu uliopita aliisaidia tena kutetea Taji lao la Ubingwa kwa kupiga Bao 20.
Majuzi Juventus walimbadili Tevez kwa kumsaini Straika wa Atletico Madrid ya Spain, Mario Mandzukic ambae anatoka Croatia.
Akithibitisha Uhamisho huu, Rais wa Boca Juniors Daniel Angelici alisema: "Ni Siku ya furaha sana na ya kuridhisha. Kurudi kwa Tevez akiwa kwenye kilele cha mafanikio ni habari njema kwa Washirika na Mashabiki wote wa Boca na Soka la Argentina!"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni