Jumanne, 3 Januari 2017


Baada ya Coastal Union kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4–1 dhidi ya Kimondo FC kwenye Uwanja wa Karume jijini  Dar, kocha wa timu hiyo, Mohamed Kampira ameibuka na kusema anatamani mechi zao zote za nyumbani zilizosalia wamalizie uwanjani hapo.


Mchezo huo wa Kundi B, ulipangwa kuchezwa uwanjani hapo ikiwemo ni sehemu ya adhabu kwa Coastal Union kucheza mechi moja nje ya uwanja wao wa nyumbani wa Mkwakwani na mbili kucheza hapo bila ya mashabiki baada ya mashabiki wake kumpiga mwamuzi walipocheza dhidi ya KMC.

Kocha huyo alidai kuwa, wanapocheza nje ya Mkwakwani ndiyo wanacheza vizuri zaidi na kupata matokeo mazuri tofauti na wanapocheza nyumbani.

“Tangu msimu huu uanze, hatujawahi kushinda wala kupata sare katika uwanja wetu wa nyumbani, tumefungwa na Polisi Morogoro, KMC na Njombe Mji, lakini tukicheza nje ya tunapata matokeo mazuri.

“Nadhani uwanja wetu wa nyumbani tunafanya vibaya  kutokana na presha ya mashabiki wetu kutaka matokeo ya haraka kiasi cha kusababisha wachezaji kushindwa  kucheza kwa kufuata maelekezo, hivyo ni bora mechi zetu zote za nyumbani tuchezee katika Uwanja wa Karume, Dar,” alisema Kampira.

Coastal Union kwa sasa inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi tisa, huku KMC ikiongoza kundi hilo ikiwa na ponti 19.

SOURCE SALEHJEMBE





Zikiwa zimebaki wiki mbili pekee kabla ya kuanza kwa Michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon), beki wa Yanga aliye na kikosi cha timu ya taifa ya Togo, Vincent Bossou ameweka bayana kwamba atapigana kwenye kombe hilo kuhakikisha kwamba anaitangaza timu yake.

Bossou ni miongoni mwa wachezaji watatu watakaoiwakilisha Ligi ya Tanzania Bara kwenye mashindano hayo yatakayofanyika nchini Gabon kuanzia Januari 14 wengine ni Bruce Kangwa wa Azam na Juuko Murshid wa Simba ambapo Togo imepangwa kundi C, ikiwa na timu za Morocco, Ivory Coast na DR Congo.

Akizungumza kutoka Senegal kilipo kikosi hicho kwenye kambi yake amesema kwamba:

“Nipo huku Senegal kabla ya kwenda Gabon kushiriki Afcon, niwaambie mashabiki wa Yanga na Tanzania kwa ujumla kuwa nimepanga kuonyesha kiwango kama nilivyokuwa huko kwa ajili ya kuitangaza ligi ya Bongo watu wanifuatilie waone moto wangu.


“Najua hilo nitalifanikisha kwa sababu nipo vizuri na bado nina kiwango kilekile nilipokuwa huko na tunaamini kwamba tunaweza kufanya vizuri katika mashindano haya kwa sababu tuna kikosi kizuri licha ya kwamba tupo kwenye kundi gumu,”alisema Bossou.

SOURCE: CHAMPIONI

Hakuna maoni: