Timu ya wachezaji wakongwe wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha
Morogoro(MUM VETERANI) imeendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu baada ya
kukubali kipigo kingine kutoka kwa Young Muslim ya mkoani hapa.
Timu hiyo inayoundwa na wachezaji wa zamani wa timu ya Chuo Kikuu
cha Wislam cha Morogoro ilikubali kipigo cha 2-0 nyumbani dhidi ya wageni Young
Muslim ambao walionekana kutawala kwa asilimia kubwa mchezo huo.
Jamal Sarah ndiye alikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za
wenyeji baada ya kuiandikia Young Muslim goli la kwanza kabla ya Said Abdallah
kutikisa tena nyavu hizo nakuipatia timu yake goli la pili na kufanya mambo
yabaki hivyo mpaka mwisho wa mchezo huo.
Mara baada ya mchezo huo Msimamizi wa timu ya Young Muslim
Ashraf Suleiman(pedo) aliipongeza timu yake kwa kupata ushindi huo wa ugenini
licha ya kukiri kwamba bado timu yake inahitaji marekebisho.
“bado tunahitaji mabadiliko makubwa katika safu yetu ya
ushambuliaji na kiungo ili kuwa na kasi zaidi ya mashamblizi na ufungaji
magoli” Alisema Suleiman(pedo).
Timu ya Young Muslim inayomilikiwa na Ashraf Suleiman(pedo)
ipo katika maandalizi kwa ajiri ya kushiriki ligi daraja la nne mkoani Morogoro
ambapo mchezo dhidi ya MUM VETERAN ni sehemu ya maandalizi hayo.
![]() |
MUM VETERANI FC wakiwa katika picha ya pamoja. pincha na Majid Yusuf |
![]() |
Timu ya Young Muslim ikipasha kabla ya mechi yao na MUM VETERANI FC . pincha na Majid Yusuf |
![]() |
Timu ya Young Muslim ikipokea maelekezo kutoka kwa kiongozi wake Ashraf Suleimani( Pedo). pincha na Majid Yusuf |
![]() |
Timu za MUM VETERANI FC na Young Muslim wakipongezana baada ya kumaliza mchezo wao wa kirafiki. pincha na Majid Yusuf |
![]() |
Young Muslim fc na MUM VETERANI FC wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mchezo wao wa kirafiki wakidumisha amani na mshikamano. pincha na Majid Yusuf |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni