Alhamisi, 13 Agosti 2015

 


Mshambuliaji mwenye vituko wa Liverpool, Mario Balotelli amesherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kuwaalika wachezaji wenzake.

Balotelli aliamua kutengeneza keki yenye jezi namba 9 ambayo huivaa anapokuwa timu ya taifa ya Italia na si ile anayovaa Liverpool.
 
Ni mwaka wa 25 sasa kwake, na wachezaji walijitokeza katika mgahawa wa Sorrento kuungana naye, baadhi wakiwa na familia zao.
Kati ya walioungana na Balotelli ni pamoja na Lucas Leiva, Mamadou Sakho, Lazar Markovic, Roberto Firmino, Divock Origi, Emre Can, Dejan Lovren na Martin Skrtel.


Wakati Manchester United wako katika juhudi kuu kuhakikisha wanambasa Pedro Rodriguez wa Barcelona, wapinzani wao wakubwa Manchester City nao wameingia vitani.

Man City wameingia vitani wakitaka kumpata nyota huyo huku kukiwa na taarifa nyingine pia wanamhitaji Karim Benzema ambaye anatakiwa na Arsenal.
Tayari Pedro amesema anaweza kuondoka Barcelona kwa kuwa inaonekana haelewani na Kocha Louis Enrique lakini uamuzi wa City kuanza kumfuatilia unaamsha vita mpya kabisa.
Tayari Man United iko tayari kutoa pauni milioni 22 kumpata, kuingia kwa City kunaweza kusababisha kupanda kwa bei ya kiungo huyo mwenye miaka 28.
Man United inataka kumchukua kwa lengo kuziba nafasi ya Angel Di Maria ambaye amekwenda PSG.
Pedro ndiye alikuwa shujaa wa Barcelona baada ya kufunga bao lililoipa Barcelona ubingwa wa Uefa Super Cup kwa kuichapa Sevilla kwa mabao 5-4.

Lionel Messi ni kiboko, yale mabao mawili aliyofunga dhidi ya Sevilla katika fainali ya Uefa Super Cup yamempafanya afikishe mabao 24 katika mechi 24 dhidi ya timu hiyo.

Hapo unajumlisha pia mechi za La Liga na Copa de Rey. Huyu mtu ni hatari!

Ukiachana na hivyo, Sevilla inakuwa timu ya pili kufungwa mabao 24 katika mechi 24, Messi pia ameifanyia hivyo Atletico Madrid.

Hakuna maoni: