RATIBA YA KOMBE LA KAGAME 2015
Julai 18, 2015
KMKM vs Telecom
APR Vs Shandy
Yanga Vs Gor Mahia
Julai 19, 2015
LLB AFC Vs Hegaan FC
Adama City Vs Malaika
Azam Vs KCCA
Julai 7, 2015
Telecom Vs Khartoum
Gor Mahia Vs KMKM
Julai 21, 2015
Shandy Vs LLB AFC
Hegaan Vs APR
Malaika Vs Azam
Julai 22, 2015
Khartoum Vs KMKM
KCCA Vs Adama City
Telecom Vs Yanga
Julai 23, 2015
Hegaan Vs Shandy
APR Vs LLB AFC
Julai 24, 2015
Khartoum Vs Gor Mahia
KMKM Vs Yanga
Julai 25, 2015
KCCA Vs Malakia
Adama City Vs Azam
Julai 26, 2015
Gor Mahia Vs Telecom
Yanga Vs Khartoum
Julai 27, 2015 MAPUMZIKO
Julai 28, 2015 ROBO FAINALI
B1 Vs A3
A1 Vs Mshindi wa tatu Bora
Julai 29, 2015
B2 Vs C2
C1 Vs A2
Julai 29, 2015 MAPUMZIKO
Julai 31, 2015 NUSU FAINALI
Mshindi 25 Vs Mshindi 26
Mshindi 23 Vs Mshindi 24
Agosti 1, 2015 MAPUMZIKO
Agosti 2, 2015
MSHINDI WA TATU NA FAINALI
Aliyefungwa 27 Vs Aliyefungwa 28
Mshindi 27 Vs Mshindi 28
FRIENDS RANGERS BAADA YA KUJIPIMA NA YANGA , YAWAFATA AZAM CHAMANZI COMPLEX KESHO "

Afisa habari wa klabu hiyo Asha Kigundula alisema kuwa, mchezo huo utafanyika asubuhi kuanzia saa 2, asubuhi.
Kigundula alisema kuwa
wameshukuru kupata mechi hiyo ambayo itaendelea kuiweka timu yao katika
mazingira mazuri kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi daraja la
kwanza.
Alisema kuwa kucheza na timu kama
Azam ni sehemu nzuri ya kukipa kikosi chao mazoezi mazuri, kwa sababu
Azam ni timu bora na inawachezaji wenye uwezo mkubwa hapa nchini.
Kigundula alisema tayari kikosi
chao kimeshacheza mechi mbili za kirafiki, dhidi ya Yanga ambapo
ilifungwa mabao 3-2, mchezo uliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Ilala
Dar es Salaam.
Mechi nyingine ambayo Friends Rangers ilicheza na timu ya Mwadui FC, timu hiyo ya Magomeni Kagera ilishinda kwa mabao 2-1.
Chanzo, shafiidauda.blogspot.com
JOEL BENDERA AIPONGEZA TFF
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara Dokta, Joel Bendera ameipongezs TFF kwa kuandaa mashindano
ya ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 13 (U-13), na maandalizi
ya timu hiyo kwa ajili ya kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika za vijana chini
ya miaka 17 zitakazofanyika mwaka 2019 nchini Tanzania.
Bendera
amesema hiyo ndiyo njia sahihi ya kuelekea kwenye mafanikio pia amepongeza
juhudi za Chama cha Soka mkoa wa Manyara na TFF kwa kuandaa kozi za makocha na
waamuzi, akisema huo ndiyo uwekezaji mkubwa katika maendeleo ya soka mkoani
Manyara.
Aidha
aliwaasa makocha kutumia mbinu za kisasa za ufundishaji soka walizozipata
kwenda kuendeleza vipaji vya wachezaji watakaowafundisha.
Pia
Bendera amewahakikishia wakazi wa Manyara atahakikisha wanaandaa vipaji
vitakvyowawezesha kuwa na timu bora itakayowakilisha mkoa wa Manyara.
MAZEMBE YAKIRI KUPOKEA OFA YA KUMUUZA UFARANSA KALABA, LAKINI KATUMBI ALETA ‘MIZENGWE’ KIBAO
KLABU ya TP Mazembe imethibitisha kupokea ofa ya klabu ya Lille ya Ufaransa kumtaka Nahodha wa Zambia, Rainford Kalaba (pichani kulia).
Mwenyekiti
wa Mazembe, Moise Katumbi amesema kwamba mabingwa hao wa Jamhuri ya
KIdemokrasia ya Kongo (DRC) wanaitathmini ofa ya Lille kwa Kalaba.
Kalaba
amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia Lille, kufuatia kocha wa
zamani wa Zambia, Herve Renard kuteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo
Ligi Kuu nchini humo, maarufu kama Ligue One Mei mwaka huu.
“Lille inamtaka Kalaba aende huko na tupo kwenye mazungumzo juu ya safari ya Lille,” amesema Katumbi.
“Sasa
tatizo ni tunataka mustakabali mzuri kwa Kalaba. Tunatazama hilo kama
Kalaba atakwenda huko ili mradi tu au kwa mustakabali mzuri.
“Unatakiwa
kuangalia mustakabali na ada ya uhamsho kwa Kalaba, kwa sababu unajua
mchezaji anapotoka Afrika wanatoa fedha kidogo na hiyo ndiyo inayoziua
timu nyingi (kwa Afrika).”
Kalaba
amekuwa mchezaji wa Mazembe tangu mwaka 2010 alipojiunga na timu hiyo
ya Lubumbashi yenye washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Samatta na
Thomas Ulimwengu kwa mkopo kutoka Sporting Braga ya Ureno, kabla ya
kusaini Mkataba wa moja kwa moja mwishoni mwa msimu wake wa kwanza DRC.
Kiungo
huyo wa Zambia alikuwa mfungaji bora wa Mazembe msimu wa 2013/2014 kwa
mabao yake tisa, akiisaidia timu ya Lubumbashi kubeba taji la nne
mfululizo na la 14 la Ligi ya DRC.
Murray kucheza raundi ya pili Wimbledon
Andy
Murray anaungana na Waingereza wenzake watatu kucheza hatua ya pili ya
michuano ya tenis ya Wimbledon inayoendelea jijini London, baada ya
kumcharaza Mikhail Kukushkin wa Kazakhstan.
Murray, wa tatu kwa
ubora duniani alishinda kwa seti 6-4 7-6 (7-3) 6-4 katika mchezo
uliodumu kwa saa mbili na dakika 13 wakati hali ya hewa ikiwa nyuzi joto
41 za Selisyasi.
Murray anasema ilikuwa mechi ngumu. Na yeye ndiye aliyeifanya iwe hivyo katika seti ya pili ya mchezo.
Kuingia
raundi ya pili Murray anaungana na Waingereza wenzake Liam Broady,
Aljaz Bedene na James Ward kutinga raundi ya pili, akiwemo pia Heather
Watson namba moja kwa ubora nchini Uingereza kwa upande wa wanawake
akimbwaga Caroline Garcia wa Ufaransa kwa seti 1-6 6-3 8-6 .
Hii
ni mara ya kwanza kwa Waingereza wanne kwa pamoja kutinga raundi ya pili
tangu mwaka 2006. Katika raundi hiyo Murray atakabiliana na Mholanzi
Robin Haase, ambaye alimbandua Alejandro Falla wa Colombia kwa seti nne.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni