STARS YA MAYANGA KUONDOKA NA WACHEZAJI 18 KWENDA KIGALI RWANDA
Kikosi kingine cha timu ya Taifa
kitaondoka nchini siku ya jumamosi kuelekea nchini Rwanda kucheza mchezo wa
kirafiki na timu ya taifa ya Rwanda katika kumbukumbu ya mauaji ya Kimbali.
Kocha Salum Mayanga ataondoka na kikosi
cha wachezaji 18 kuelekea nchini Rwanda kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki,
akisaidiwa na kocha Bakari Shime.
KABURU KUONGOZA MSAFARA WA TAIFA STARS KUELEKEA ETHIOPIA, MISRI
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania
(Taifa Stars) Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kilichoondoka jana
jioni kwenda Addis Ababa nchini Ethiopia kuweka kambi ya wiki moja kujiandaa
na mchezo dhidi ya Misri.
Msafara wa Taifa Stars utaongozwa na Wajumbe
wa Kamati ya Utendaji, Vedastus Lufano na Geofrey Irick Nyange “Kaburu” ambaye pia ni Makamu Rais wa klabu ya Simba.
Mchezo kati ya Misri na Tanzania
unatarajiwa kuchezwa Juni 14, katika uwanja wa Borg El Arab jijini Alexandria,
ikiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika (AFCON)
mwaka 2017.
Kikosi cha Stars kiliondoka saa 11 jioni
kwa Shirika la ndege la Ethiopia ambapo inatarajiwa kuwasili jiji la Addis
Ababa majira ya saa 1 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Wachezaji wanaosafiri kuelekea nchini
Ethiopia ni Deogratias Munish, Aishi Manula, Mwadini Ali, walinzi Shomari
Kapombe, Oscar Joshua, Erasto Nyoni, Nadir Haroub, Aggrey Morris, Mwinyi Haji,
Salum Mbonde na Juma Abdul.
Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda,
Salum Telela, Frank Domayo, Jonas Mkude, Said Ndemla, washambuliaji Saimon
Msuva, John Bocco, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta,Mrisho Ngasa na Juma
Liuzio.
Naye mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF Vedastus Lufano amesema timu inakwenda kuweka kambi Ethiopia kwa ajili ya kupambana katika mchezo dhidi ya Misri.
Afisa wa FIFA akiri alipokea mrungula!

Wizara
ya Sheria ya Marekani imechapisha taarifa inayoelezea jinsi Afisa wa
zamani wa FIFA Chuck Blazer alivyokiri kuwa yeye pamoja na wenzake
walipokea rushwa ikiwa ni pamoja kuichagua Afrika Kusini kuwa mwenyeji
wa fainali ya kombe la dunia mwaka 2010.
Katika taarifa hiyo
imeweka wazi mtandao wa malipo ya rushwa ulivyokuwa ukifanywa ndani ya
shirikisho la soka duniani FIFA, taarifa zinazoegemea uchunguzi
uliofanywa na shirika la kijasusi la Marekani FBI.
Taarifa hiyo
ambayo inamwelezea Afisa humo wa zamani wa Fifa Chuck Blazer kukiri
kupokea rushwa sasa huenda ikaibua mengi kwenye kashfa ya rushwa
inayoindamana shirikisho la FIFA.
Mmerakani huyo kwenye taarifa
hiyo inadai alikuwa ni mmoja wa watu waliosuka mipango ya kupokea rushwa
katika tukio jingine la fainali la kombe la dunia 1998.
Taarifa
za Kukiri zipo katika maandishi wakati wa kesi yake mwaka 2013 wakati
kesi yake ilipokuwa akisikilizwa katika mahakama ya Easten New York huko
Marekani ambapo alikiri makosa kumi yaliyokuwa yanamkabili.
Blazer
alikuwa afisa wa ngazi juu wa FIFA eneo la kanda ya Amerika Kaskazini
na Kati na ukanda wa nchi Caribbean kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2011.
Marekani
imefungua kesi ya rushwa inayowakabili maafisa wa FIFA jambo
lililofanya Rais wa FIFA Sepp Blatter kuamua kutangaza kujiuzulu.
Mwendesha
mashtaka wa Marekani wiki iliyopita aliwashtaki maafisa 14 wa ngazi wa
juu wa FIFA tuhuma za rushwa, kutakatisha fesha,
Afrika Kusini yakana kutoa hongo kwa FIFA

Afrika kusini
Afrika kusini imekana kwa mara nyengine tena kwamba ilitoa hongo ili kupewa maandalizi ya kombe la dunia la mwaka 2010.
Waziri wa michezo nchini humo Fikile Mbalula, amewaambia wanahabari
kwamba Afrika kusini itashirikiana na wachunguzi kutoka Marekani lakini
imekataa kuingizwa katikati ya ugomvi kati ya FIFA na Marekani.
Amesema kuwa dola millioni 10 zilizotolewa zilikuwa malipo ya kusaidia
soka miongoni mwa raia wa Afrika wanaoishi katika visiwa vya Caribbean
na yalilipwa miaka kadhaa baada ya michuano hiyo kuandaliwa na Afrika
kusini.
Benitez ndio kocha mpya wa Real Madrid
Aliyekuwa kocha wa Napoli Rafa Benitez amethibitishwa kuwa k ocha wa Real Madrid katika kandarasi ya miaka mitatu.
Benitez
mwenye umri wa miaka 55 anachukua mahala pake Carlo Ancelotti ambaye
aliondoka katika kilabu hiyo miezi 12 tu baada ya kuisaidia kushinda
kombe lao la kumi la vilabu bingwa Ulaya.
Benitez ambaye ni
mzaliwa wa Madrid amehudumu misimu miwili kama mkufunzi wa Napoli ,baada
kufanikiwa na vilabu kadhaa vya Ulaya.
Baada ya kuisaidia
Valencia kushinda kombe la Uefa mwaka 2004,mwaka unaofuatia alielekea
Liverpool na kuisaidia kilabu hiyo kushinda kombe la vilabu bingwa ikiwa
ni msimu wake wa kwanza katika kilabu hiyo ya Mersyside.
Miaka
miwili baadaye aliisaidia Liverpool kufika katika fainali za kombe la
vilabu bingwa Ulaya na mwaka 2013 alikuwa kaimu mkufunzi wa Chelsea
waliposhinda kombe la Yuropa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni