Ijumaa, 14 Agosti 2015

NANI NI NANI LIGI KUUU VODACOM ( VPL)2015/2016

16:00YANGAVs    AZAM FC

16:00TANZANIAVs    NIGERIA

Msimamo wa Ligi Kuu Msimu Huu

RnTimuPWDLFAGdPts
1AFRICAN SPORT00000000
2Azam FC00000000
3Coastal Union00000000
4JKT RUVU00000000
5KAGERA SUGAR00000000
6MAJIMAJI FC00000000
7MBEYA CITY00000000
8MGAMBO SHOOTING00000000
9MTIBWA SUGAR00000000
10MWADUI FC00000000
11NDANDA FC00000000
12SIMBA SC00000000
13STAND UNITED00000000
14T. PRISONS00000000
15TOTO AFRICANS00000000
16YANGA00000000


Kesho Jumapili Yanga inacheza mechi ya kirafiki na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya katika kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika kikosi cha Yanga, yumo kiungo mshambuliaji Deus Kaseke aliyesajiliwa hivi karibuni kutoka Mbeya City, ambaye angeweza kuutumia mchezo huo kuwaaga wachezaji wenzake.

Pengine Kaseke angecheza kipindi cha kwanza akiwa Mbeya City kisha kipindi cha pili akacheza Yanga kama alivyofanya Geoffrey Mwashiuya pindi timu yake ya zamani ya Kimondo ilipocheza na mabingwa hao watetezi wa ligi kuu.

Kaseke amesema kuwa, haoni sababu ya kuichezea Mbeya City kwani tayari yeye ni mchezaji wa Yanga na hawezi kuichezea timu nyingine.

“Nicheze Mbeya City? Hapana, nitacheza Yanga kwa dakika zote tena kwa kiwango changu kilekile, watu wasitarajie kwamba nitazitumikia timu zote kwa vipindi tofauti. Waelewe tu kuwa mimi ni mchezaji wa Yanga.

“Wachezaji wengi hasa wa kimataifa wamekuwa wakifanya hivyo, lakini kwangu sijafikiria,” alisema Kaseke ambaye amejihakikishia namba kwenye kikosi cha Yanga.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi, alisema: “Nilikuwa Dar es Salaam, ndiyo narudi Mbeya sasa (jana), nitaiandaa timu kesho (leo Jumamosi) kwa mechi hiyo.”


Katika mchezo huo, Yanga inatarajiwa kuwatumia nyota wake wengine wapya akiwemo Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Malimi Busungu, Simon Matheo, Benedict Tinocco na Haji Mwinyi.


Yanga ipo kambini jijini Mbeya kwenye baridi kali lakini kocha wa timu hiyo, Hans van Der Pluijm anaamini hali hiyo ya hewa itawaweka fiti wachezaji wake kuweza kufanya vizuri katika mechi zao zijazo ikiwemo dhidi ya Azam FC.

Agosti 22, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga itacheza na Azam mechi ya Ngao ya Jamii ambayo hukutanisha timu bingwa wa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara na iliyoshika nafasi ya pili.
Yanga ambayo ni bingwa mtetezi ipo kambini Mbeya ambako kesho Jumapili itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine ili kujipima nguvu.

Pluijm, amesema: “Licha ya kuwepo baridi, naamini hiyo ni njia mojawapo ya kuwajenga wachezaji wangu huku tukihakikisha tunapunguza makosa yanayojitokeza mara kwa mara kwenye kikosini chetu.”

Tayari Yanga imecheza mechi mbili za kirafiki ikiwa Nyanda za Juu, Kusini na kushinda zote ikianza kwa kuitandika Kimondo kwa mabao 4-1 kabla ya kuituliza Prisons kwa mabao 2-0.

Imebakiza mechi moja dhidi ya Mbeya City ambayo ndiyo timu ngumu zaidi katika ukanda huo.


Kiungo Justice Majabvi, amesaini mkataba wa kuichezea Simba na amepiga mkwara mzito kwa viungo wenzake akiwemo Jonas Mkude kuwa wajipange la sivyo watakaa benchi.

Awali, baadhi ya viongozi wa Simba hawakutaka kabisa Majabvi asajiliwe kwa maelezo kuwa kiwango chake ni cha kawaida wakati wapo wazawa kama Mkude, Said Ndemla, Awadh Juma na Abdi Banda wanaoweza kucheza nafasi yake.

Lakini Kocha Dylan Kerr akawaambia viongozi hao: “Mimi ndiye bosi na lazima mumsajili Majabvi.” Kweli Majabvi raia wa Zimbabwe akasaini mkataba wa miaka miwili na sasa ni mali ya Simba.

Muda mfupi baada ya kusaini mkataba huo, Majabvi akasisitiza: “Najipanga kikamilifu kucheza kikosi cha kwanza, nimekuta watu wanacheza hapa nami nitapambana ili nicheze, naamini hakuna linaloshindikana.


“Kwa upande wangu ninajipanga kikamilifu kuhakikisha napigana na kuonyesha uwezo wangu wa hali ya juu ambao utamshawishi kocha anipange katika kikosi cha kwanza na kuwapokonya namba hawa niliowakuta,” alisema Majabvi ambaye amewahi kuichezea timu ya Vicem Hai Phong ya Vietnam.


Kama ulidhani Carlo Ancelotti ana maisha ya shida sana kwa kuwa alifukuzwa kazi Real Madrid, basi umejidanganya.
Kocha huyo ametupia picha mtandaoni akionyesha bonge la samaki alilolivua kule Vancouver nchini Canada.



Ancelotti raia wa Italia amekuwa akisafiri nchini mbalimbali akila maisha kwa raha zake licha ya kwamba Madrid waliotesha majani kibarua chake na kumkabidhi Rafa Benitez.


Siku chache baada ya kutwaa ubingwa wa Uefa Super Cup, Barcelona wamekiona cha moto baada ya kukutana na kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Athletic Bilbao.

Licha ya kuwemo kwa nyota Lionel Messi, Bilbao wametoa adhabu hiyo kwa Barcelona katika mechi ya Super Cup ya Hispania.

Hadi mapumziko, Bilbao walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Mikel San Jose aliyefunga katika dakika ya 13.

Huku ikionekana Barcelona ingerejea na kujirekebisha katika kipindi cha pili kama ilivyofanya kwenye mechi ya Uefa Super Cup dhidi ya Sevilla baada ya kutangulia kufungwa na kusawazisha, haikuwa hivyo.

Kwani Bilbao ndiyo walizidi kupaa na kufunga mabao ya harakaharaka baada ya Artiz Aduriz kufanya mabao mawili ya fasta katika dakika ya 53 na baadaye 63.

Kitendo cha Bilbao kufikisha mabao matatu kilionekana kuwachanganya Barcelona, wakaendelea kushambulia mfululizo na kujisahau kufanya ulinzi mzuri.

Hali hiyo ilisababisha Bilbao kupata bao la nne kupitia Aduriz aliyekuwa anafunga lake la tatu au hat trick.

vyanzo vya habari salehjembe & azam chama langu

KAMPUNI ya Azam Media leo imezindua rasmi chaneli yake mpya yenye ubora wa juu kabisa, iitwayo “Azam Sports HD”.Tangu kuanza kwa huduma za AzamTV, wateja wamekuwa wakijiuliza hasa ni kipi wanachopata kutokana na alama ya HD iliyo mbele ya kisimbuzi – kuanzia sasa watabaini. 
Baada ya miezi 18 ya mipango na uwekezaji, leo umeshuhudiwa uzinduzi wa chanel ya kwanza itakayowezesha wateja kufaidi picha na sauti zaubora wa juu kabisa “HD” kutokana na teknolojia ya kiwango cha juu. 
Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam TV, Tido Mhando akizungumza katika hafla hiyo


Mtendaji Mkuu wa Azam TV, Rhys Torrington akizungumza katika hafla hiyo

Waalikwa mbalimbali wakifuatilia zoezi hilo
Wateja wa kifurushi chenye chaneli mpya ya “Azam Sports” wataweza kuona timu zao wazipendazo katika VPL katika picha ang’avu zaidi ambazo hazijawahi kuonekana. 
Zaidi, kampuni pia imetangaza rasmi ujio wa Ligi Kuu ya Hispania maarufu La Liga ambayo wateja wataipata katika ubora wa HD kupitia Chanel mpya. Mchezo wa kwanza kuoneshwa katika msimu mpya wa La Liga 2015/16, ni Malaga dhidi ya  Seville wa Ijumaa Agosti 21, 2015 na timu zote vigogo zitakuwa zikicheza na kuoneshwa Live mwisho wa juma lijalo, na kila mzunguko wa msimu mzima katika ubora wa HD. 
Mkuu wa Idara ya Masoko ya Azam Media, Mgope Kiwanga akizungumza wakati wa hafla hiyo


Waalikwa mbalimbali wakati wa zoezi hilo leo

Maofisa wa Azam TV wakijadiliana mambo wakati wa shughuli hiyo

Kifurushi kinachojumuisha chaneli ya Azam Sports HD kitaonekana kwa watazamaji wa AzamTV wa Tanzania pekee ambao wanalipia kifurushi chochote kati ya vitatu vya sasa; Pure, Plus au Play – na nyongeza ya ya SH15,000 kwa mwezi, ikijumuisha VAT. 
Pamoja na chaneli mpya ya Azam Sports HD, malipo hayo yatajumujisha chaneli za klabu za Manchester United, Liverpool na Real Madrid  ambazo kwa sasa ni sehemu ya kifurushi cha  Azam Play. 
Kadhalika malipo ya mwezi kwa kifurushi cha Play kitapunguzwa hadi Tsh25,000 kuanzia sasa. Kwa wale wasiokuwa na luninga zenye uwezo wa kuona picha za HD au waya maalum wa HD (HDMI), watapata chaneli mpya na kufuatilia La Liga na mengineyo – japo si kwa ubora wa HD.  
Pia kwa wateja wasiohitaji kujiunga na kiufurushi kipya hawapaswi kuwa na wasiwasi wa kutoona michezo ya VPL kwani itaendelea kuoneshwa kupitia  Azam One na Azam Two kama ilivyokuwa kabla – Jambo lililo tofauti ni kuwa michezo yenye mvuto zaidi itaoneshwa pia kwenye Azam Sports HD.
Zaidi ya La Liga na VPL, Azam Sports HD itakuwa na vipindi mbalimbali vya kimichezo  vitakavyojumuisha michezo ya Ligi za soka za Uganda, Kenya na, Burundi – itakayoanza hivi karibuni.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington amesema “Uzinduzi wa Azam Sports HD ni hatua kubwa katika maendeleo ya AzamTV. 
Mwenyeki wa klabu ya Azam FC, Sheikh Said Muhammad alikuwepo


Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC, Said Tuliy kulia na Collin Frisch kushoto

Hata kabla ya ya kuanza mwaka 2013 tulijipanga kukidhi mahitaji ya teknolojia kwa ajili ya kutoa picha za ubora wa  HD ili kutuwezesha baadaye kumpatia mtazamaji picha bora zaidi bila kulazimika kununua vifaa vipya. Jambo ambalo hatukulitazamia ni kutekeleza hilo ndani ya muda mfupi – na kuanzisha chaneli  kwa kuonesha moja kwa moja soka la La Liga! Ambalo ni bora zaidi barani Ulaya. Uwezo wa kuona moja kwa moja na katika HD timu mzipendazo huko Hispania na kwa VPL, pamoja na vipindi vingine vya michezo kutoka sehemu mablimbali duniani, unatoa chaguo muhimu na ambalo wateja wetu wanalimudu. Huu ni mwanzo tu – jiandae kwa makubwa zaidi” 



Mourinho:Daktari'mjinga' hatakuwepo uwanjani


Dakta Eva Carneiro amehudumu Stamford bridge kwa miaka 5 sasa

Meneja wa Chelsea manager Jose Mourinho amekariri msimamo wake dhidi ya kitengo cha utabibu cha timu yake.
Mourinho aliwakaripia Dakta Eva Carneiro na Jon Fearn kwa kuingia uwanjani huku timu hiyo ikisalia na wachezaji wachache kufuatia kufurushwa kwa kipa nambari moja Thibaut Courtois katika mechi ngumu ya kufungua msimu kati yao na Swansea .

Bi Carneiro aliingia uwanjani katika muda wa lala salama kumtibu kiungo wa Chelsea Eden Hazard

Bi Carneiro aliingia uwanjani katika muda wa lala salama kumtibu kiungo wa Chelsea Eden Hazard ambaye alionekana kagongwa kifundo cha mguu.
'The special one' alisema kuwa daktari mkuu Carneiro na msaidizi wake Fearn hawatakuwa uwanjani Chelsea itakapokuwa ikipambana na Manchester City siku ya jumapili.

Carneiro aliwakilishwa katika mkutano huo na mawakili wake kutoka kwa kampuni ya mawakili ya Mishcon de Reya.

''Hii haimaanishi kuwa hawatakuwepo siku nyingine ,katika siku za usoni'' alisema Mourinho.
Kocha huyo aliyasema hayo baada ya kukutana na kitengo kizima cha utabibu cha Chelsea siku ya Alhamisi.
Carneiro aliwakilishwa katika mkutano huo na mawakili wake kutoka kwa kampuni ya mawakili ya Mishcon de Reya.

Mourinho amekariri kuwa Daktari 'mjinga' hatakuwepo uwanjani

Mourinho aliwataja Carneiro na Fearn kuwa 'wajinga' baada yao kuingia uwanjani kumtibu Hazard katika dakika za lala salama ya mechi ya kufungua msimu.
Kutokana na shinikizo la wapinzani wao Mourinho aliona kuwa kumuondoa Hazard katika kipindi hicho kuliwasaidia wapinzani wao kuwa na wachezaji wawili zaidi hivyo kuwazidi nguvu.

Mourinho alisema hajuti kuwaita ''wajinga''

Mourinho alipoulizwa iwapo anauhusiano mzuri na na kitengo hicho cha utabibu alisema kuwa
''Mimi nao tunahusiana kama kawaida tu vile ''

Mourinho amesema kuwa uhusiano wao ni wa wazi na kuwa haoni kosa la matamshi yake

'Wenyewe wamenieleza kuwa hawajawahi kushabikiwa zaidi ya kipindi hichi nilipoingia Chelsea''
''Walinieleza kuwa wanahitaji kukosolewa ili na wao wajiendeleze''

Kombe la dunia:Timu 3 za Afrika zashindwa



Uganda ililazwa na New Zealand

Timu tatu kutoka Afrika ziliambulia kichapo katika kombe la dunia la mpira wa pete inayoendelea Sydney Australia.
Wawakilishi wa Afrika Mashariki ,Uganda, waliambulia kibano cha alama 76-33 mikononi mwa New Zealand katika hatua ya nusu fainali huko Sydney.
Kufuatia kushindwa huko Uganda sasa inajiunga na Afrika Kusini na Malawi ambazo pia hazikuwa na siku nzuri.
Afrika kusini ilikuwa imechapwa alama 62-46na Uingereza.

Afrika kusini ilikuwa imechapwa alama 62-46na Uingereza.

Malawi kwa upande wake itajilaumu yenyewe kwa kuboronga katika muda wa lala salama wa mechi hiyo baada ya kushindwa na Jamaica kwa alama moja pekee.
Malawi ilikuwa uongozini hadi dakika ya mwisho safu ya ulinzi ilipozembea na kuiruhusu Jamaica kufunga bao la kusawazisha na kisha kuwapiku.
Kufuatia kichapo hicho cha alama moja Malawi walishindwa kufuzu kwa mkumbo wa nusu fainali ya mashindano hayo.

Mataifa hayo ya Afrika yamesalia kuwania nafasi ya 5 hadi 16.

Mkufunzi wa Malawi Mary Waya ameiambia BBC michezo kuwa timu yake ndiyo iliyokuwa bora ila ilikosea tu ilipowadia wakati wa kuwa wakakamavu kisaikolojia.
Kufuatia matokeo hayo sasa Mataifa hayo ya Afrika yamesalia kuwania nafasi ya 5 hadi 16.
Mashindano hayo yanaendelea.