Jumanne, 31 Machi 2015
Jumatano, 25 Machi 2015
leo tena
Tambwe siri
ya mabao
Tambwe alisema kasi waliyonayo sasa imechangiwa kwa kiasi kikubwa na hali ya utulivu iliyopo kwa timu hivi sasa jambo linalowafanya wacheze bila presha na umakini mkubwa.
Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe ametoa siri ya safu ya
ushambuliaji ya timu hiyo kufanya vyema kwenye mechi mbalimbali za hivi
karibuni.
Tambwe alisema kasi waliyonayo sasa imechangiwa kwa kiasi
kikubwa na hali ya utulivu iliyopo kwa timu hivi sasa jambo linalowafanya
wacheze bila presha na umakini mkubwa.
Alisema mchezaji anapokuwa na mambo yanayomvuruga nje au
hata ndani ya uwanja, anaondoka mchezoni na kama mshambuliaji ndiyo hujikuta
wanakosa mabao mengi ya wazi kutokana na kutokuwa sawa kisaikolojia.
Tambwe aliongeza kuwa jambo lingine linalowafanya wacheze
vizuri kwa sasa ni umoja na ushirikiano uliopo baina ya wachezaji wa timu hiyo
pamoja na kila mtu kutekeleze majukumu yake ndani na nje ya uwanja.
“Viungo na mabeki wanafanya kazi nzuri kuhakikisha tunafunga
mabao. Hili ni jambo ambalo linatuhamasisha washambuliaji tupambane ili ufunga
mabao mengi tusiwachoshe wenzetu ambao wanafanya kazi kubwa kuzuia tusifungwe
na kutuchezesha,” alisema Tambwe.
Tambwe alimsifu Kocha wa Yanga, Hans Pluijm kwa jinsi
alivyoweza kubadilisha kiwango cha wachezaji wa timu hiyo ndani ya kipindi
kifupi na amekuwa akiwalea kama watoto wake jambo linalofanya wazidi kuwa na
kiu ya kufanya vizuri. Katika hatua nyingine Tambwe alisema Simba itamlipa
fedha zake wakati wowote kutoka sasa.
“Viongozi wa Simba wamewasiliana na mimi ili waanze mchakato
wa kunilipa, ni jambo la kushukuru kwa kuwa waungwana kwenye suala hili,”
alisema Tambwe
Mbeya City
kucheza na vigogo
Mbeya City iliyopoteza makali yake ya msimu uliopita kwa
sasa ipo katika nafasi ya tisa ikiwa na pointi 23, imebakiwa na michezo saba
kati ya hiyo italazimika kupata matokeo mazuri dhidi ya Azam, Yanga na Simba
ndani ya siku 11.
Mbeya City itabidi ifanye kazi ya ziada kuhakikisha inabaki
kwenye Ligi Kuu Bara kwani inakutana na mechi tatu ngumu ndani ya siku 11.
Mbeya City iliyopoteza makali yake ya msimu uliopita kwa
sasa ipo katika nafasi ya tisa ikiwa na pointi 23, imebakiwa na michezo saba
kati ya hiyo italazimika kupata matokeo mazuri dhidi ya Azam, Yanga na Simba
ndani ya siku 11.
Mbeya City itacheza na Azam Aprili 8 kisha itaikabili Yanga
Aprili 11 mechi zote zitachezwa jijini Dar es Salaam itamaliza na Simba Aprili
18 kwenye Uwanja wa Sokoine. Baada ya kumaliza mechi hizo Mbeya City itaikabili
Kagera Sugar, Prisons na Polisi Morogoro mechi hizo zote zitachezwa kwenye
Uwanja wake wa nyumbani wa Sokoine Mbeya.
Kocha wa timu hiyo Juma Mwambusi alikiri kuwa anakabilriwa
na hali ngumu kwa kuzikabili timu hizo tatu kubwa kwenye Ligi Kuu Bara, lakini
wamejiandaa kwa lolote.
“Kweli si mchezo kukutana na timu tatu kubwa kwa muda mfupi
na ukiangalia wao wanapambana juu kutwaa ubingwa wakati sisi huku tunatafuta
nafasi ya kubaki kwenye ligi, tumejiandaa na tunaendelea
kujiandaa kwa ajili ya mechi zote zilizo mbele yetu na
hatuna hofu, tutapambana na tutajua mwisho itakuaje,” alisema Mwambusi
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)