Jumamosi, 22 Aprili 2017



Simba Sports Club
D'salaam, Tanzania 
22/4/2017.

           TAARIFA KWA UMMA

Klabu Ya Simba SC inapenda kuwajulisha wanachama na wapenzi wake kuwa  imesitisha maandamano iliyopanga kuyafanya Jumanne wiki ijayo 25.04.2017 , baada ya nia na dhamira njema ya serikali kutaka kushughulikia sintofahamu inayoendelea baina ya klabu na Shirikisho la Soka nchi (TFF). 

Ikumbukwe jana klabu yetu , ililiandikia  barua Jeshi la Polisi nchini ikiomba kibali cha maandamano ya amani, yaliyopangwa kuhudhuriwa na viongozi,wanachama na washabiki wa klabu yetu kwenda Wizara inayosimamia Michezo nchini, yakiwa na lengo la  kupeleleka kilio chetu juu ya namna TFF inavyoshughulikia    malalamiko ya muda mrefu na ya sasa ya klabu hii kubwa nchini. 

Katika barua iliyoandikwa na katibu Mkuu wa Baraza la michezo nchini (BMT) Mohammed Kiganja kwa niaba ya Serikali, imetutaka Shirikisho na Klabu kutafuta namna sahihi na iliyo na weledi katika kushughulikia changamoto hizi zinazoweza kuvuruga amani ya nchi. 

Serikali kupitia barua hiyo,imeahidi pia kutukutanisha pande zote haraka iwezekanavyo,ili kwa pamoja tumalize sintofahamu hii kwa maslahi ya mchezo wa mpira wa miguu Tanzania.

Klabu ya Simba inachukua nafasi hii ya kipekee kuishukuru serekali kupitia baraza la michezo la taifa ( BMT) kwa hatua mahsusi na za haraka katika kutafuta suluhisho la kudumu la jambo hili.


Tunawaomba wanachama na washabiki wetu watulie na sote tuache majibizano yoyote ili kutoa fursa kwa Serikali kusimamia kikamilifu jambo hili. 

Klabu ya Simba inafanya mawasiliano  na Jeshi la Polisi nchini kuwajulisha kusudio letu la kusitisha maandamano hayo. 

IMETOLEWA NA... 

Haji S Manara 
Mkuu wa Habari wa Simba Sc

Simba nguvu moja
(chanzo sallehjembe)


Chelsea yaivuruga Tottenham kombe la FA       

Chelsea iliizaba Tottenham mabao 4-2 na hivyobasi kujikatia tiketi katika fainali ya kombe hilo dhidi ya mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Arsenal dhidi ya Manchester City.  Chelsea iliizaba Tottenham mabao 4-2 na hivyobasi kujikatia tiketi katika fainali ya kombe hilo dhidi ya mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Arsenal dhidi ya Manchester City.                
Mchezaji wa Chelsea Nemanja Matic alifunga bao zuri kutoka mbali na kuisaidia timu yake kuinyamazisha Tottenham katika nusu fainali ya Kombe la FA katika uwanja wa Wembley.

Chelsea iliizaba Tottenham mabao 4-2 na hivyobasi kujikatia tiketi katika fainali ya kombe hilo dhidi ya mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Arsenal dhidi ya Manchester City.

Willlian aliiweka mbele Chelsea kunako dakika ya sita kwa kupiga mkwaju
 wa adhabu kabla ya kuongeza la pili kwa njia ya penalti kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.
Harry Kane alikuwa amesawazisha kutoka kwa krosi iliopigwa na Christian Ericksen kwa Suprs ambao walisawazisha tena kupitia bao la Delle Ali.

Mchezaji wa ziada Eden Hazard aliiweka Chelsea mbele kwa mara ya tatu kabla ya Matic kufunga bao la nne na kuiweka kifua mbele Chelsea.
 
(chanzo bbc michezo)


Jumapili, 8 Januari 2017

4G NDANI YA ZANZIBAR , AZAMU 4 YANGA 0




Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva amesema wamekikubali kipigo kutoka Azam FC lakini bado wana nafasi ya kujirekebisha.

Yanga imepokea kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Azam FC katika mechi ya mwisho ya Kundi B katika michuano ya Mapinduzi. Mechi hiyo imechezwa jana kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Msuva amesema mashabiki wasikate tamaa, waendelee kuwaunga mkono nao kupitia benchi la ufundi na wao wenyewe watajirekebisha.

"Mpira una matokeo matatu, kushinda, sare au kufungwa. Kufungwa imetutokea sisi, lakini hatuna ujanja. Nawaomba mashabiki wasikate tamaa na badala yake waendelee kutuunga mkono.

"Benchi la ufundi wameona makosa yetu, sisi wachezaji tumeona na tutayafanyia kazi na kuendelea kufanya vizuri.

"Unajua kikubwa ambacho ni kizuri tumevuka kwenda nusu fainali hivyo tuna nafasi ya kujirekebisha kwenye nusu fainali na ikiwezekana fainali," alisema.






Baada ya Yanga kupoteza kwa mabao 4-0 dhidi ya Azam FC, Simba imesema itaendelea kuchukua tahadhari kubwa kwa kila mechi yake ya Kombe la Mapinduzi.

Simba imeshinda mechi zake zote za Mapinduzi lakini haikuwa ikishinda kwa idadi kubwa ya mabao kama ilivyo kwa Yanga.

Simba inashuka dimbani Amaan mjini Zanzibar kuivaa Jang’ombe Boys katika michuano hiyo.

Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema wako tayari na wanachotaka ni kufanya vizuri.

“Kila mechi ni mechi nyingine, lazima kuwa makini kwa lengo la kufanya vizuri,” alisema.

Simba inaongoza Kundi A ikiwa na pointi saba baada ya kushinda mbili na sare moja.


Iwapo itashinda leo, uhakika asilimia mia kuivaa Yanga katika nusu fainali utakuwa umepatikana.
 
SOURCE SALEHJEMBE


Jumanne, 3 Januari 2017


Baada ya Coastal Union kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4–1 dhidi ya Kimondo FC kwenye Uwanja wa Karume jijini  Dar, kocha wa timu hiyo, Mohamed Kampira ameibuka na kusema anatamani mechi zao zote za nyumbani zilizosalia wamalizie uwanjani hapo.


Mchezo huo wa Kundi B, ulipangwa kuchezwa uwanjani hapo ikiwemo ni sehemu ya adhabu kwa Coastal Union kucheza mechi moja nje ya uwanja wao wa nyumbani wa Mkwakwani na mbili kucheza hapo bila ya mashabiki baada ya mashabiki wake kumpiga mwamuzi walipocheza dhidi ya KMC.

Kocha huyo alidai kuwa, wanapocheza nje ya Mkwakwani ndiyo wanacheza vizuri zaidi na kupata matokeo mazuri tofauti na wanapocheza nyumbani.

“Tangu msimu huu uanze, hatujawahi kushinda wala kupata sare katika uwanja wetu wa nyumbani, tumefungwa na Polisi Morogoro, KMC na Njombe Mji, lakini tukicheza nje ya tunapata matokeo mazuri.

“Nadhani uwanja wetu wa nyumbani tunafanya vibaya  kutokana na presha ya mashabiki wetu kutaka matokeo ya haraka kiasi cha kusababisha wachezaji kushindwa  kucheza kwa kufuata maelekezo, hivyo ni bora mechi zetu zote za nyumbani tuchezee katika Uwanja wa Karume, Dar,” alisema Kampira.

Coastal Union kwa sasa inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi tisa, huku KMC ikiongoza kundi hilo ikiwa na ponti 19.

SOURCE SALEHJEMBE





Zikiwa zimebaki wiki mbili pekee kabla ya kuanza kwa Michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon), beki wa Yanga aliye na kikosi cha timu ya taifa ya Togo, Vincent Bossou ameweka bayana kwamba atapigana kwenye kombe hilo kuhakikisha kwamba anaitangaza timu yake.

Bossou ni miongoni mwa wachezaji watatu watakaoiwakilisha Ligi ya Tanzania Bara kwenye mashindano hayo yatakayofanyika nchini Gabon kuanzia Januari 14 wengine ni Bruce Kangwa wa Azam na Juuko Murshid wa Simba ambapo Togo imepangwa kundi C, ikiwa na timu za Morocco, Ivory Coast na DR Congo.

Akizungumza kutoka Senegal kilipo kikosi hicho kwenye kambi yake amesema kwamba:

“Nipo huku Senegal kabla ya kwenda Gabon kushiriki Afcon, niwaambie mashabiki wa Yanga na Tanzania kwa ujumla kuwa nimepanga kuonyesha kiwango kama nilivyokuwa huko kwa ajili ya kuitangaza ligi ya Bongo watu wanifuatilie waone moto wangu.


“Najua hilo nitalifanikisha kwa sababu nipo vizuri na bado nina kiwango kilekile nilipokuwa huko na tunaamini kwamba tunaweza kufanya vizuri katika mashindano haya kwa sababu tuna kikosi kizuri licha ya kwamba tupo kwenye kundi gumu,”alisema Bossou.

SOURCE: CHAMPIONI

Jumanne, 7 Juni 2016

HII NDO ILIKUWA FAINALI ZA RADIO MUM CUP ( 91.1FM)


VIJANA WA ASTASHAADA MUM WA BEBA UBINGWA WA RADIO MUM CUP JUMAPILI YA WIKI JANA !

HABARI PICHA ZA MATUKIO YA MECHI YA FAINALI YA RADIO MUM CUP





Vijana wa Cheti














Baadhi ya wachezaji wa Timu ya mwaka wa pili wakijipanga kuzuia fauru ya kuelekea langoni kwao. picha na Majid Yusuf.

Vijana wa Cheti wakishangilia goli la pekee lililowapa ushindi dhidi ya Mwaka wa 2 Jumapili ya wiki jana. picha na Majid Yusuf.




















Jumamosi, 7 Mei 2016

CBE DODOMA WAIKUBALI MUM FC



Na Majid  Yusuf, MUM
Timu ya  mpira wa miguu ya Chuo Kikuu cha Waislam Morogoro(MUM FC) imeendelea kufanya vizuri katika michezo ya kirafiki baada ya kuibuka na ushindi wa moja bila dhidi ya Chuo Kikuu cha Biashara Dodoma (CBE FC).

Katika mchezo huo uliochezwa Jumamosi ya leo katika Chuo Kikuu cha Waislam Morogoro ( MUM) ulishuhudiwa wenyeji MUM FC wakitafuta mbinu ya ziada ili kupata ushindi baada ya wageni CBE Dodoma kuonekana kuimalika hukuwakihitaji kulipiza kisasi dhidi ya timu hiyoiliyowachabanga 4 - 3 huko kwao mkoani Dodoma.

Shukurani za pekee ziende kwa timu kaptain wa MUM FC Mohamed Humbaru( Bro Mudy)aloipatia goli la ushindi na kufanya mchezo umalizike kwa moja bila dhidi ya wapinzani wao CBE FC ya Dodoma.


Mara baada ya mchezo huo walimuwa timu zote mbiliwalipongezana kutokana na timu hizokuonyesha mchezowa kiungwana uliokuwa umesheheni nidhamu kuanzia ule wa mkoani Dodoma na wa leo. 

HABARI PICHA
Kocha mkuu wa MUM FC Abdallah Kessy akijipanga kukabiliana na mtanange wa CBE  jion ya leo. picha na Majid Yusuf.


Kocha mkuu wa MUM fc akiufatilia mtanange mkali dhidi yake na CBE ya Dodoma.  picha na Majid Yusuf.

Timu ya MUM FC akifanya mazoezi madogo kabla ya mechi yao  na CBE ya Dodoma. picha na Majid Yusuf.



MUM FC  wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao waleo jion dhidi ya CBE FC ya Dodoma. picha na Majid Yusuf




Timu ya CBE ya Dodoma wakifanya womapu kabla ya mechi yao dhidi ya wenyeji wake MUM FC jion ya leo. picha na Majid Yusuf.


CBE FC wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi yao na MUM FC. picha na Majid Yusuf.

Benchi la ufundi la MUM FC wakifatilia mtanange wao na CBE ya Dodoma jion ya leo. picha na Majid Yusuf.





Kocha wa MUM FC akitoa maelekezo kwa timu yake dhidi ya CBE FC ya Dodoma. picha na Majid Yusuf




Baadhi ya wachezaji wa timu ya MUM FC wakijipongeza baada ya goli la kwanza la Mohamed  Humbaru. picha na Majid Yusuf.

Baadhi ya mashabiki wakiufatilia kwa makini  mtanange wa MUM FC dhidi  ya CBE ya Dodoma  jioni ya leo.  picha na Majid Yusuf.

Benci la ufundi la timu ya CBE YA Dodoma wakifatilia mtanange kwa umakini. picha na Majid Yusuf.


Timu zote mbili CBE FC na MUM FC wakiwa katika picha ya pamoja  baada ya mchezo wao ulopigwa katika viwanja vya MUM kwa ishara ya kudumisha upendo na amani. picha na Majid Yusuf.


Waziri wa michezo MUM  mstaafuwa Hussein Nyombi(kulia)  akitambulisha uongozi mpya kwa wageni CBE. Picha na Majid Yusuf.